KATIBU Tawala wilaya ya Nyamagana Thomas Salala amezindua duka jipya la simu aina ya Tecno huku akitoa wito kwa watumiaji wa vitendea kazi hivyo kutumia kujiletea maendeleo yao.
Wito huo ameutoa leo jijini Mwanza wakati wa tukio la Kampuni hiyo kuonesha bidhaa zao wanazozalisha za simu za Tecno ambapo kiongozi huyo amemwakikisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi.
Alisema serikali ya awamu ya sita inathamini michango inayofanywa na Tasisi Binafsi hapa nchini katika jitihada za kila siku za kujiletea maendeleo hivyo akawaomba waweze kukopesha wananchi wa kipato cha hali ya chini na wanafunzi simu hizo kwa riba ndogo.
“Taasisi Binafsi zinatoa Mchango Mkubwa kuingiza Pato la Taifa kwa kulipa kodi hivyo tuziunge mkono kwa kununua bidhaa zao” alisema Salala.
Aidha, Salala alisema matumizi ya simu yana faida kubwa kijamii na kiuchumi hivyo aliwataka watumiaji kutumia kwa manufaa hayo.
Naye Erick Msaki ambaye ni mmoja wapo wa wateja waliopata Huduma ya kununua simu alisema amepata kwa bei rafiki hivyo kuwaomba wananchi wenzake kununua simu hizo.