Home Kitaifa WANANCHI WAENDELEA KUKUMBUSHWA KUCHANGIA NGUVU KAZI UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI MUSOMA...

WANANCHI WAENDELEA KUKUMBUSHWA KUCHANGIA NGUVU KAZI UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa jimbo la Musoma Vijijini wamekumbushwa kuendelea kuchangia nguvu kazi katika ujenzi wa shule za sekondari unaoendelea kwenye maeneo yao.

Ukumbusho huo umetolewa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo aliotoa leo februari 18 kwenda kwa wananchi.

Amesema jimbo la Musoma Vijijini lenye jumla ya Kata 21 lina sekondari 26 za Kata zikiwa za serikali na 2 za binafsi.

Muhongo amesema sekondari 3 zinazojengwa na serikali kuu ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika februari 28 katika Kijiji cha Butata Kata ya Bukima,Kijijini Kasoma Kata ya Nyamrandirira na Kijiji cha Kurwaki Kata ya Mugango

Amesema wanavijiji kwenye maeneo hayo wamekubali kuchangia nguvukazi zao kwenye ujenzi wa sekondari hizo na wengine wameendelea kukumbushwa.

” Elimu bado ni kipaumbele chetu na tunaendelea kuwakumbusha wanavijiji kwenye maeneo ya ujenzi kuendelea kuchangia nguvu kazi.

” Tunaishukuru sana serikali kuu kwa kuendelea kutuletea fedha nyingi kwaajili ya ujenzi wa shule kwenye vijiji vyetu,amesema.

Mbunge huyo amesema sekondari 9 zinajengwa kwa kutumia nguvukazi na michango ya fedha kutoka kwa wanavijiji wazaliwa wa vijiji vyenye ujenzi na viongozi vyao

Amesema Kijiji cha Muhoji Kata ya Bugwema shule itafunguliwa 28 Feb 2025 na ujenzi unakamilishwa Kisiwa cha Rukuba Kata ya Etaro,Kijiji cha Mmahare Kata ya Etaro,Kijiji cha Nyasaungu Kata ya Ifulifu,Kijiji cha Kiriba Kata ya Kiriba,Kijiji cha Kataryo Kata ya Tegeruka,Kijiji cha Musanja Kata ya Musanja,Kijiji cha Chitare Kata ya Makojo na Kijiji cha Nyambono Kata ya Nyambono

Aidha mbunge huyo ameendelea kuwambusha wadau mbalimbali wa elimu kukaribia kwenye jimbo hilo na kuchangia sekta ya elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!