Na Magreth Mbinga
Wananchi wa Wilaya ya Temeke na maeneo ya jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao katika zoezi la afya chek ambalo linafanyika katika hospitari ya Rufaa ya Mkoa Temeke ambalo linafanyika bila malipo kwa muda wa siku tatu kuanzia leo septemba 9 hadi 11.
Hayo yamezungumzwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sadath Mtware wakati akifungua zoezi hilo litakalo wawezesha wananchi kupata vipimo bila malipo .
“Naomba mufahamu ndugu wananchi hakuna swala litakuwa ghali kama afya kwahiyo linapoandaliwa zoezi la afya unahitaji fedha tuwashukuru wadau wetu kwa kutuwezesha kufanikisha zoezi hili“amesema Mtware.
Pia Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dk Joseph Kimaro amesema wapo wadau waliowapatia dawa,vifaa tiba ,vitenganishi kwaajili ya maabara ili watu waweze kupata huduma .
“Zoezi hili linawatu wengi nyuma yake na tunawashukuru sana wadau wote walioweza kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha kwamba wananchi wa Temeke wanapata huduma za kibingwa za kupimwa pamoja na tiba” amesema Dk Kimaro.
Sanjari na hayo Meneja Mkuu wa Consolation medicare Sevelian Christopha amesema wameamua kuunga mkono afya cheki kwaajili ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Wilaya ya Temeke na Hospitali ya Temeke .
“Lengo la kuja kusapoti na watu wafahamu bidhaa zetu na mahali ambapo tunapatikana tinamashine ya kupima moyo ya kisasa kabisa ambayo haitamsababishia maumivu mgonjwa wakati akitoka kupima “amesema Sevelian.
Aidha Nickson Biarushengo kutokea Morah Pharmaceticals ambao ni wadhamini katika tukio hilo amesema wanazo dawa za aina mbalimbali kutoka india na kusema kuwa wamefurahia kushiriki katika afya cheki inasaidia wao kama kampuni kuwawezesha wagonjwa mbalimbali kuelewa dawa zao na kuzitambua ,kutumia na kupata kuelewa zaidi.
“Leo tumelenga dawa za meno na kinywa tunayo yavkusukutua kinywa kama fizi zinatoka damu itazuia na itazuia maambukizi yanayotoka mdomoni“amesema Biarushengo.