Kutoka Kagera 28/9/2022
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ametoa wito kwa wananchi waliopo katika maeneo ya mpakani mwa Uganda na Tanzania kuchukua tahadhari wakati Serikali inaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya tishio la ugonjwa wa Ebola.
Prof. Makubi ametoa wito huo leo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera, baada ya kutuma timu ya wataalam kutoka Wizara ya afya na kukutana na viongozi wa mkoa ili kujionea utayari wa kukabiliana ugonjwa huo uliotokea nchi ya jirani.
Prof. Makubi ameeleza kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hapa nchini.