Home Kitaifa WANANCHI WA HANANG WAMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA

WANANCHI WA HANANG WAMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA

NA. MWANDISHI WETU

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang wameishukuru Serikali kutokana na juhudi kubwa iliyozifanya katika urejeshaji wa hali na misaada ya kibinadamu iliyotolewa kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe kutoka Mlima Hanang.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama alipokagua kujionea hatua za urejeshaji wa hali katika maeneo yaliyoathirika katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang leo tarehe 20 Disemba, 2023.

Akitoa shukrani kwa Serikali Mchungaji Martine Tarimo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna walivyoratibu zoezi la urejeshaji wa hali kwa waathirika wa maafa yaliyotokea Wilayani humo na kueleza wataendelea kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika kusaidia waathirika wa maafa hayo.

“Tumeona msaada wa Serikali tangu siku ya kwanza ya madhila ya Maporomoko ya Mawe na Matope, serikali imekaa na sisi na imetusikiliza na hoja tulizotoa zimefanyiwa kazi kwa wakati,” alifafanua Mchungaji Tarimo

Akizungumza kuhusu urejeshaji wa hali, Mkazi wa Katesh Bw, Ibrahim Mwenda alisema kwa hatua hiyo wataendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha wanarejea katika hali zao za awali huku akiendelea kuishukuru Serikali.

“Tunaomba sisi kama wafanyabiashara tusiendele tena kufanya shughuli zetu hapa, tunaomba tupelekwe eneo jingine rafiki kwa shughuli zetu,” aliomba.

Naye Mkazi wa Kijiji cha Gendabi Bi. Julian Masay ameishukuru serikali kwa ufuatiliaji wa kila siku hasa katika kipindi hiki ambacho wamekubwa na madhila ya Maafa na kueleza wameendelea kupata faraja kwa namna Serikali na wadau mbalimbali walivyojitokeza katika kusaidi hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!