Maelfu ya Wananchi jijini Dar es salaam, leo Septemba 01, 2022, wameendelea kutoa maoni mbalimbali kuhusu umuhimu wa Tozo katika maendeleo, Wengi wakieleza namna Tozo zilivyosaidia na zinavyoedelea kusaidia katika kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma bora za msingi.
“Tulikuwa na mashaka kidogo kuhusu hizi Tozo, lakini baada ya kuwasikiliza viongozi wetu jana, tumeelewa Tozo hizi zinafanya nini, umuhimu wake ni upi, na zitatisaidaje katika kuboresha maisha yetu na wananchi wote kwa ujumla” – Wananchi
Hata hivyo, Baadhi ya waliotoa maoni, wameeleza kushangazwa kwao na Wananchi wachache kuwa na mtazamo tofauti juu ya Tozo, na kuhoji kwamba tukiwasikiliza hao wachache, Vituo vya Afya, Barabara, Shule na kadhalika, vitajengwa na fedha zipi?