Home Kitaifa WANANCHI SINGA WAIOMBA SERIKALI DHAMANA KUHUDUMIA MAJI KIJIJINI KWAO

WANANCHI SINGA WAIOMBA SERIKALI DHAMANA KUHUDUMIA MAJI KIJIJINI KWAO

Ashrack Miraji Kilimanjaro

Mwenyekiti wa kitongoji Cha Singa Juu, Ignas Mallya ameyasema hayo wakati akiongoza kikao cha wananchi kwa lengo la kuwachagua wawakilisha watatu watakao wawakilishi kwenye kamati mpya ya bodi ya maji katika kijiji hicho chenye vitongoji vinne Singa Chini, Kati, Kifueni na Singa Juu vya Kata ya Kibosho wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro.

“Niiombe Serikali iweze kutusaidia sisi wananchi wa kijiji Cha Singa kuhusu suala la Maji katika kijiji chetu, tumekuwa na changamoto kubwa hasa katika kulipia maji ambayo yanatokana na nguvu kazi zetu kuanzisha chanzo cha maji kwenye Kijiji chetu.Kuna watu wengi wamepoteza maisha na wengine kutoa ardhi zao ili maji yaweze kupita bila ya kulipwa fidia yoyote hadi sasa”

“Huduma ya maji ni huduma ya kila mwananchi hivyo tulikuwa tunaiomba serikali kutokana na nyakati za sasa kuazishwa bodi za maji kupitia Halmashauri kuwa na jukumu ziweze kusimamia huduma za maji vijijini,basi kijiji chetu kiwe na Kamati ambayo inasimamia maji na kuingiza mapato kwenye Kijiji chetu. Nimeteseka kipindi kirefu maana tulikuwa na kamati ya maji hapa kijijini ambayo ilikuwa haifanyi kazi Kwa wakati na kusikiliza kero za wananchi hususani kwenye huduma ya maji” amesema Ignas Mallya.

Mwenyekiti Mallya aliendelea kusema “nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipo washukuru wadau wa maendeleo hasa kijana wetu, Joseph Mushi amekuwa mtu wa watu mpenda maendeleo katika kijiji hiki na kutusaidia mambo mbalimbali ya kiuchumi na kututaka pia tuchague kamati makini ya maji, itakuwa chachu ya maendeleo katika Kijiji chetu na kutatua matatizo na kusimamia huduma ya maji hapa Singa”

Kikao hicho kimechagua wajumbe watatu katika vitongoji vinne il kwenda kuungana na vitongoji vingine ambao wapo kwenye kijiji hicho kupata wajumbe tisa watawawakilisha wananchi kwenye bodi ya maji ambayo imeudwa na serikali (Sikika) lengo pia ni kutaka kuishauri Serikali juu ya usimamizi wa maji katika kijiji chetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!