Na.Elimu ya Afya kwa Umma.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Mhe.Judith Nguli ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo kutumia fursa ya Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani kuchunguza Afya bure pamoja na kushiriki katika mazoezi ili kujikinga na Magonjwa Yasiyoambukiza.
Mhe. Nguli amesema hayo Ofisini kwake Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro mara baada ya kufanya Kikao na Timu kutoka Wizara ya Afya,Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Mvomero ikiwa ni katika Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani Tarehe 7,April, 202