Home Kitaifa WANANCHI MUSOMA WAFURAHIA ” OFFER” YA MUWASA KUREJESHEWA MAJI BILA FAINI

WANANCHI MUSOMA WAFURAHIA ” OFFER” YA MUWASA KUREJESHEWA MAJI BILA FAINI

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI Wilaya ya Musoma wameshukuru na kufurahia nafuu ya kurejeshewa huduma ya maji iliyotolewa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Musoma ” MUWASA”.

Wakizungumza na Mzawa Blog wananchi waliositishiwa huduma hiyo wamesema nafuu iliyotolewa itawafanya kurejesha maji na kuendelea na huduma.

Tatu Juma mkazi wa Majita Road ambaye kwa muda amesitishiwa huduma kutoka na kushindwa kulipa kwa muda amesema anakwenda ofisi za MUWASA kukamilisha taratibu.

Amesema deni lake limekuwa kubwa kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zilipelekea kushindwa kulipa kwa wakati.

Tatu amesema tangazo lililotolewa na MUWASA kuhusu kurejeshewa huduma ya maji bila faini na kuingia mkataba wa kulipa taratibu amelisikia na anakwenda kukamilisha taratibu.

” Niwashukuru sana MUWASA kwa utaratibu walioutoa ambao unakwenda kutusaidia kurejesha maji.

” Maji ni huduma muhimu kuwepo nyumbani na hiki ambacho wamekifanya MUWASA tunasema nj asante kwao”,amesema.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Musoma “MUWASA” Nicas Mugisha amesema ni wajibu kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanapata huduma ya maji.

Amesema nafuu iliyotolewa itakwenda hadi januari 20 na kuwataka wananchi waliositishiwa huduma ya maji muitumia fursa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!