Home Afya WANANCHI MARA WATAKIWA KUTUMIA FURSA UJIO WA MADAKTARI BINGWA 45 WA DKT.SAMIA

WANANCHI MARA WATAKIWA KUTUMIA FURSA UJIO WA MADAKTARI BINGWA 45 WA DKT.SAMIA

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI kutoka halmashauri 9 za mkoa wa Mara wametakiwa kutumia fursa za ujio wa madaktari bingwa 45 wa Rais Dkt.Samia kupata matibabu.

Kauli hiyo imetolewa leo juni 24 na mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Enock Mtambi wakati wa hafla ya mapokezi ya madaktari hao kwenye ukumbi wa uwekezaji uliopo kwenye ofisi yake.

Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anawajali wananchi na kutambua umuhimu wa afya zao na ndio kilichopelekea kuanzishwa kwa program hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kwa siku 5 watakazokuwepo madaktari hao kwenye halmashauri zote 9 wananchi wenye changamoto za afya wafike kwenye hospital na vituo vya afya ili wakutane na madaktari hao.

Hii ni fursa ambayo imekuja kwenye mkoa wetu tulioletewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na wananchi wanapaswa kuitumia, Niwaombe wananchi wafike kwenye hospital na vituo vya afya ili waweze kukutana na madaktari bingwa na kupata matibabu ya kibingwa“, amesema Mtambi.

Amesema mkoa umewapokea madaktari hao na kuwahakikishia kutekeleza majukumu yao kama ilivyopangwa na kuwataka waganga wa wilaya kuwapa ushirikiano kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake Mganga wa manispaa ya Musoma Dk.Mustafa Waziri kwa niaba ya waganga wa wilaya amesema wamepokea maelekezo ya mkuu wa mkoa na wanakwenda kutoa ushirikiano kwa madaktari hao.

Naye mratibu wa huduma za madaktari bingwa wa Rais Dkt.Samia kutoka Wizara ya Afya Joachim Masunga amesema moja ya lengo la ujio wa madaktari hao ni kuwapunguzia gharama wananchi za huduma za kibingwa kwa kuwafikia kwenye maeneo yao.

Amesema madaktari hao pia watawajengea uwezo madaktari na wahudumu wengine wa afya kwenye hospital na vituo vya afya watakapo kuwepo mkoa wa Mara.

Daktari bingwa mshauri mwandamizi wa ” Mama Samia Mentorship Program ” Dk.Suleim Charles Muttani atakayekuwepo hospital ya Musoma vijijini amesema wapo tayari kuwahudumia wananchi katika changamoto zao za afya walizo nazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!