Home Afya WANANCHI MARA WAFURAHIA HUDUMA YA UPIMAJI WA AFYA NA USHAURI MAENEO YAO

WANANCHI MARA WAFURAHIA HUDUMA YA UPIMAJI WA AFYA NA USHAURI MAENEO YAO

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI mkoani Mara wamepokea na kushukuru huduma ya upimaji wa afya na ushauri kwenye maeneo yao.

Huduma hiyo ni agizo la serikali na mkoa wa Mara umeanza kutekeleza kwenye wilaya zake katika kuwahudumia wananchi.

Wakizungumza na Mzawa Blog eneo la Musoma bus manispaa ya Musoma wakati wa upimaji wa magonjwa ya macho na ushauri wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza wamesema hilo ni jambo jema lililoanzishwa.

Wamesema wapo wananchi ambao wanakuwa wazito kufika vituo vya afya na hospital kujua hali zao afya hivyo huduma hiyo imekuja kuwasaidia.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Maswi Warioba amesema amefika eneo la huduma na kupimwa macho na kupewa ushauri wa kufuata.

Amesema amekuwa akisumbuliwa na macho kuwasha lakini hajawahi kufika hospitalini lakini kupitia huduma hiyo ya mtaani amepima na kupata ushauri.

” Tunashukuru ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kutoa maelekezo ya huduma hii na tumeona wataalamu wameanza kutufikia”,amesema Maswi.

Mratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mkoa wa Mara Ester Muya amesema magonjwa ya macho ni sehemu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yaapaswa kupatiwa matibabu mapema.

Amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa yasiyo na vimelea vinavyoweza kusambazwa.

Akizungumzia magonjwa ya afya ya akili ambayo huazimishwa kila oktoba 10 amesema wagonjwa hao hawapaswi kunyanyapaliwa bali wahudumiwe kama wagonjwa wengine.

Amesema lengo la kupeleka huduma mtaani ni kuongeza uelewa kwa jamii juu ya magonjwa ya afya ya akili na kuwataka vijana kuachana na kutumia vilevi na madawa ya kulevya ili kukabiliana na afya ya akili.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Mara Saidi Mtanda alisema wananchi wenye magonjwa ya muda mrefu wanaopitia changamoto watafuatwa maeneo yao na kuwea kupatiwa huduma za afya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!