
Na Shomari Binda-Musoma
WANANCHI wa Kisiwa cha Rukuba kilichopo Musoma Vijijini wameishukuru serikali kwa kufikiwa na miradi mbalimbali ukiwemo wa umemejua.
Wakizungumza kisiwani hapo kwa nyakati tofauti na Mzawa Blog leo februari 23/2025 wamesema kisiwa hicho kwa sasa kimebadilika na maendeleo yanskwenda kwa kasi.
Wamesema katika siku za hivi karibuni wameshuhudia miradi ya afya,elimu na mingine ikiwafikia kwa juhudi za serikali na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo.
Mmoja wa wananchi hao Jumbe Kibago ambaya pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Musoma Vijijini amesema serikali chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuwafikia kimaendeleo wananchi wa Kisiwa cha Rukuba.
” Tunaishukuru sana serikali ambayo inapeleka kwa kasi maendeleo kwenye Kisiwa cha Rukuba kuanzia afya,elimu na hata masuala ya nishati ta umeme.
” Mbunge wetu Profesa Sospeter Muhongo nae amekuwa mstari wa mbele kusikuma maendeleo hayo nae tunamshukuru sana kwa jitihada zake”,amesema.
Katika taarifa iliyotolewa leo jumapili februari 23 na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo imesema kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba kimefungiwa umemejua (solar energy) wa thamani ya shilingi milioni 345.6 kwaajili ya mwanga na utoaji huduma wakati wote.
Taarifa hiyo imesema sehemu nyingine za Kisiwa hicho zitafungiwa umemejua (solar energy) kupitia mradi mkubwa wa kufungia umemejua kwenye Visiwa vya nchi nzima vilivyoko Bahari ya Indi na Maziwa makuu.
Sehemu ya hiyo imedai kuwa Kisiwa cha Rukuba nacho kiko ndani ya mradi ambao matayarisho yake yanakamilishwa ikiwa ni taarifa kutoka REA kwenda kwa Mbunge wa Jimbo.
” Maji ya bomba Kisiwani kwetu
baada ya umemejua kusambazwa Kisiwani Rukuba RUWASA itaendelea na mradi wake wa kusambaza maji ya bomba Kisiwani humo
“Elimu Kisiwani
Kisiwa cha Rukuba kina shule ya Msingi yenye maktaba na nyumba za makazi ya walimu wote upungufu wa vyumba vya madarasa haupo na sekondari mpya inajengwa Kisiwani humo na imepangwa ifunguiliwe mwaka huu, 2025.
“Kituo cha fya kimeanza kutoa huduma za matibabu ambapo kituo hiki kimefungiwa umemejua (solar energy)”imesema sehemu ya taarifa hiyo.
