Na Shomari Binda-Musoma
WANANCHI wa Kijiji cha Muhoji Kata ya Bugwema jimbo la Musoma vijijini wamejipanga kufumgua shule ya sekondari hapo mwakani.
Ujenzi wa awali unaokamilishwa ni vyumba 2 vya madarasa, ofisi 1 ya walimu, Pamoja na vyoo matundu 12 ya wavulana,matundu 12 ya wasichana na matundu 2 ya walimu.
Wachangiaji wakuu wa ujenzi wa Muhoji sekondari ni wananchi wa Kijiji cha Muhoji. Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kupitia fedha zake na mfuko wa jimbo.
Hadi sasa ujenzi ukiendelea bado halmashauri ya Musoma jaijachangia ujenzi wa shule hiyo yenye lengo la kupunguza umbali wa wanafunzi kwenda masomoni.
Wananchi wameiomba TARURA wakati ujenzi ukiendelea isaidie ukamilishaji wa ujenzi wa barabara linaloingia Muhoji sekondari likitokea barabara kuu la Murangi- Masinono-Manyamanyama (Bunda).
Muhoji Sekondari itakuwa ni eekondari ya pili ya Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne (Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji).
Sekondari moja (Bugwema Sekondari) kwa Kata hii haitoshi, matatizo makuu yakiwa ni umbali mrefu wa kutembea kwa baadhi ya wanafunzi na mirundikano madarasani
Wazaliwa au watu wenye chimbuko la Kata ya Bugwema wanaombwa waungane na ndugu zao kukamilisha ujenzi wa Muhoji Sekondari.
Wadau wengine wa maendeleo wanaombwa sana wachangie ujenzi wa shule hii.
Michango ya fedha ielekezwe kwenye benki ya NMB kwa akaunti namba 30302301062
jina serikali ya Kijiji cha Muhoji.