Home Kitaifa WANANCHI KATA YA KAMNYONGE WAMUOMBA DC CHIKOKA KULIFUNGUA SOKO LAO

WANANCHI KATA YA KAMNYONGE WAMUOMBA DC CHIKOKA KULIFUNGUA SOKO LAO

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa Kata ya Kamnyonge manispaa ya Musoma wamemuomba mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kufanya jitihada ya kufungua soko lao.

Wakitoa kero na maswali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Majita Road wamesema moja ya eneo ambalo ni kero kwao ni kuona soko hilo halifanyi kazi.

Wamesema licha ya uzuri wa soko hilo lakini lieshindwa kufanya kazi kwa wafanyabiashara kushindwa kuingia kwenye soko hilo na kufanya biashara.

Mmoja wa wananchi hao Juma Charles amesema huenda ujio wa mkuu huyo wa Wilaya ikawa bsraka ya kuboreshwa kwa soko hilo.

Amesema ikiwezekana soko hilo liwe maalum kama soko la kuku au mbuzi ambalo litapelekea kuchangamka na kuwavutia wafanyabiashara wengi zaidi.

Licha ya maombi ya soko hilo kwa mkuu huyo wa Wilaya wananchi hao wamefikisha kero na maswali mbalimbali yakiwemo ya afya,elimu na miundombinu.

Diwani wa Kata ya Kamnyonge Devid Cosmas amemuomba Mkuu wa Wilaya kutoa maelekezo juu ya soko hilo ikiwa ni pamoja na kulifanya kama soko maalum la ukusanyaji wa samaki.

Akijibu na kufafanua masuala mbalimbali mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema Musoma lazima iwe ya kibiashara na lazima atalifatlia soko hilo.

Amesema ziara zake za mtaa kwa mtaa zimemsidia na atakutana na mkurugenzi na afisa biashara ili kuona soko hilo linafunguliwa.

Amesema lipo suala la uvuvi haramu ambalo limepelekea kupotea kwa samaki na kuahidi kupambana vilivyo na uvuvi haramu.

Aidha mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kulipa kupaumbele suala la elimu na kuiomba kila kaya kuchangia katika uboreshaji wa elimu.

” Ndugu zangu wananchi wa Kamnyonge niwaambie hakuna kitu kilicho bora kama elimu na tusione tabu kuchangia ikiwemo walimu wa ziada.

” Yamezungumwa mengi lakini ushauri wangu tusiue kesho ya vijana wetu maana elimu ndio kipaumbele chetu lakini mambo mengine yaliyozungumzwa yatafanyiwa kazi”,amesema.

Akizungumzia suala la usafi amesema Manispaa ya Musoma inakuja na kampeni ya kung’alisha mji hivyo kuweka utaratibu wa uchangiaji wa usafi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!