Home Kitaifa WANANCHI KATA YA BUHARE WASHUKURU KUPATA DARAJA

WANANCHI KATA YA BUHARE WASHUKURU KUPATA DARAJA

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa Kata ya Buhare iliyopo manispaa ya Musoma wameishukuru serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kwa ujenzi wa daraja linalowaunganisha

Wakizungumza na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo alipotembelea daraja hilo linalounganisha Kata hiyo na Kata ya Makoko.

Wamesema licha ya kuunganisha Kata hizo lakini pia kukamilika kwa daraja hilo kutamaliza changamoto zikiwemo za wanafunzi kupita kwenda shuleni.

Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Masatu Malima,amesema licha ya daraja hilo lakini yapo mengi yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na barabara kupitika

Mhandisi msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo linalogharimu zaidi ya milioni 300 na barabara zinazoroka Simon Joseph amesema daraja hilo lipo hatua za mwisho kukamilika ili wananchi waweze kulitumia.

Diwani wa Kata ya Buhare,Jumbula Rugola,amesema mambo mengi mazuri yamefanyika na kuishukuru serikali pamoja na mbunge kwa ufatiliaji wake wa miradi ya maendeleo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Buhare Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema kazi aliyonayo ni kupeleka maendeleo kwa wananchi.

Amesema changamoto ya kuvuka kwenda Kata ya Makoko zinakwisha kufuatia ujenzi wa daraja na barabara nyingi zimefunguliwa na wananchi kupita kwa raha.

Ninachopigania kwa sasa ni kupatikana kwa kituo cba afya ambacho mambo yote ya kiafya yaishie hapa hapa Buhare na hilo nitalifanikisha.“”

“Lingine ni kuhakukisha huduma ya maji inapatikana kwa kila mwananchi nyumbani kwake ns nimeshaonges na wstu wa Muwasa”, amesema

Mbunge huyo amesema baada ya kufanyika kwa miradi mingi ya maendeleo sasa ni zamu ya kuwezeshana kiuchumi ili maisha yaendelee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!