Home Kitaifa WANANCHI JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI WAMSHUKURU WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWATEMBELEA

WANANCHI JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI WAMSHUKURU WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWATEMBELEA

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI katika jimbo la Musoma vijijini wamemshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuwatembelea na kuahidi kuendelea kujengwa kwa kiwango cha lami Barabara ya Musoma-Makojo hadi Busekera yenye kilometa 92.

Shukrani hizo zimetolewa na mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo kwa niaba ya wananchi hao.

Amesema wanapaswa kumshukuru Waziri Mkuu na serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwatembelea na kuahidi kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Waziri Mkuu katika ziara yake kwenye jimbo hilo aliwaeleza wana-Musoma Vijijini kuhusu uamuzi wa serikali wa kuendelea kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye vijiji vyao.

Waziri Mkuu aliyasema hayo kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika Kijijini Bwai Kwitururu, Musoma Vijijini siku ya Alhamisi februari 29.

Kwenye shukrani hizo Muhongo amesema tayari kilomita 5 zimeshawekewa lami na barabara hiyo imo keenye bajeti ya mwaka huu (2023/2024)
na kibali kimetolewa barabara litangazwe na mkandarasi apatikane ili aendelee na ujenzi.

“Tunamshukuru sana Waziri Mkuu kututembelea kwenye jimbo letu na ilikuwa ni ziara yenye mafanikio makubwa na wananchi wameifurahia”

“Tunawaomba viongozi wengine wa kitaifa waje kitutembelea kwani wananchi wa Musoma vijijini ni wakalimu na wanapenda wageni” amesema Muhongo.

Aidha amesema Wana-Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za kufadhili miradi ya maendeleo.

“Tunamshukuru sana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kututembelea jimboni na kwa kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo ambayo ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020-2025” ameongeza

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!