Na Shomari Binda-Tarime
WADAU wa micezo wilayani Tarime mkoani Mara wamempongeza mbunge wa viti maalum Esther Matiko kwa kuandaa mashindano makubwa na ya mfano.
Wakizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shamba la bibi Tarime mjini wamesema licha ya kuibua vipaji mashindano hayo yatazalisha ajira.
Wamesema mashindano hayo ni makubwa na yatauchangamsha mji wa Tarime kwa kipindi chote yanapo fanyika
Akizindua mashindano hayo mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele amempongeza mbunge Estber Matiko kupitia Matiko Foundation kuzindua Matiko cup kwani michezo ni afya,ajira na starehe.
Amesema yeye kama mkuu wa Wilaya na viongozi wengine watatoa ushirikiano kwenye kipindi chote cha mashindano hayo.
Kwa upande wake mbunge Esther Matiko ameahidi zawadi mbalimbali kwa washindi katika fainali ambapo mshindi wa kwanza kwa upande wa soka atapata milioni 15,mshindi wa pili medali ya fedha na shilingi milioni 10,mshindi wa tatu medali ya Shaba na shilingi milioni 5 na mshindi wa nne atapata milioni 2.
Mchezaji bora atapata kiatu cha dhahabu na shilingi laki 2,kipa bora atapata groves ya dhahabu na shilingi laki 2,timu bora itapata laki 5 pamoja na kipa bora atapata shilingi laki 5.
Aidha katika uzinduzi huo imefanyika michezo mbali mbali mingi huku zikitolewa zawadi zikiwemo jezi kwa timu 20 kwaajili ya kuanza mechi leo januari 4 katika viwanja mbali mbali vya mipira vipatavyo 10 huku akitoa nyavu za magori na vifaa kwa watu wa huduma ya kwanza