Home Kitaifa WANAKUNDI LA MAENDELEO RWAMISHENYE WAMUUNGA MKONO BIBI ALIYEKWAMA KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA...

WANAKUNDI LA MAENDELEO RWAMISHENYE WAMUUNGA MKONO BIBI ALIYEKWAMA KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA 2 ZA KUISHI WATOTO YATIMA

Na Theophilida Felician Kagera.

Ikiwa ni siku chache tuu bibi mlezi wa watoto yatima kituo cha UYACHO kilichopo kata Hamgembe Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Saada Seleman kujitokeza akiililia nakuiomba Serikali wadau na jamii kumsaidia vifaa vya kukamilisha ujenzi wa nyumba mbili za kuishi watoto yatima anaowalea baadhi ya wanakundi la MAENDELEO YA RWAMISHENYE Manispaa ya Bukoba wamejichanga changa nakumfikia bibi huyo kwa msaada wa saruji.

Wanakundi hao wakihamasishwa na Katibu wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi kata hiyo ya Rwamishenye Ndugu Imani Sudi Hussen wameguswa na kilio cha bibi huyo aliye kwama ujenzi wa nyumba hizo za watoto hivyo wakawiwa nakujikusanya kwa chochote nakumshika mkono kwa mifuko sita ya saruji hiyo.

Katibu Iman akiambatana na baadhi ya wana kundi hadi kwenye kituo cha awali UYACHO amemweleza bibi kuwa kilichowapelekea kufika kwa bibi huyo nikwamba siku chache zilizopita waliona habari kwenye Group lao la WhatsApp kupitia Blog hii ya Mzawa baada yakuchapisha habari ikimuhusu bibi huyo akitoa kilio cha kuomba msaada wa vifaa vya kukamilisha ujenzi wanyumba hizo kutokea eneo husika anakozijenga Misenyi.

“Baada yakuona habari hiyo yenye kuwahusu wadogo zetu hawa tukaguswa kama hivi tulivyokufikia kwa hiki kidogo ili pengine kiweze kuongeza nguvu sehemu ya ujenzi” ameleeza katibu Iman.

Amepongeza jitihada za mlezi huyo kwajinsi anavyojitoa nakuwalea watoto yatima kwa muda mrefu kwani sikazi nyepesi.

Iman amemuahidi bibi Saada kuwa wao kama kundi wataendelea kuwa naye kwa namna watakavyokuwa wamejaliwa.

Amewasihi watoto kusoma kwa bidii ili elimu iweze kuwasaidia maisha yao ya mbeleni.

Hata hivyo ametoa wito akiiomba Serikali, wadau na jamii kwa ujumla kufanya jitihada za kumuunga mkono bibi Saada ili aweze kukamilisha ujenzi wa nyumba za watoto.

Vile vile Iman ameongoza dua yakumuombea kwa MwenyeziMungu amjalie afya njema yenye kumwezesha nguvu yakuendelea kuwasaidia watoto hao.

Nao baadhi ya wanakundi walioambatana na katibu huyo wameshukuru nakupongeza kazi kubwa ya bibi anayoifanya ya kuwalea watoto yatima ambapo wamemuhakikishia kuwa naye bega kwa bega pale panapo wezekana.

Kwa upande wake Bibi amewashukuru wanakundi hilo kwa jinsi walivyojitolea nakumfikia kituoni hapo.

“Nawashukuru sana sana mnisaidie nyumba za wadogo zenu hawa zimekwama ujenzi wake mpaka sasa hapa nilipo sina msaada hapa nilipo ni mlemevu wa miguu natambaa nimezeheka mnisaidie mnisaidie jamani” amesisitiza bibi Saada Seleman.

Bibi huyo mwenye umri wamiaka 89 anawalea watoto 290 kwenye kituo chake cha mwanzo UYACHO anaowapokea kutoka ustawi wa jamii hivyo ameanzisha ujenzi wa nyumba hizo baada ya idadi ya watoto kuwa kubwa katika kituo hicho.

Nyumba hizo ambazo moja niya watoto wakiume na nyingine ya watoto wakike anazijenga kitongoji cha Katongo, Kijiji cha Mbale Kata Kitobo Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera.

Nyumba ya watoto wakiume kwa mjibu wa maelezo yake inapungukiwa mabati, milango, madirisha na ya watoto wakike ikikwama ikiwa kwenye msingi.

Ameendelea kupaza sauti akiiomba Serikali wadau kumsaidia ili akamilishe majengo hayo.

Watoto wenyewe wame washukuru wanakundi hilo kwa kitendo cha kuguswa na hali ya changamoto ya mlezi wao ya kukwama kwa nyumba zakuishi wao wamewaomba na watu wengine kufuata nyao za wanakundi hilo na kuwachangia chochote zaidi nyumba zao zikamilike na waweze kuishi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!