Home Kitaifa WANAKIJIJI WAANZA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA DAVID MASSAMBA MEMORIAL KUSOGEZA...

WANAKIJIJI WAANZA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA DAVID MASSAMBA MEMORIAL KUSOGEZA ELIMU JIRANI

Na Shomari Binda-Musoma

WAKAZI wa Kijiji cha Kurwaki Kata ya Mugango wameanza ujenzi wa shule ya “David Massamba Memorial Secondary School” kusogeza elimu jirani.

Sekondari hii ambayo itakuwa ya pili kwa Kata ya Mugango inajengwa ikiwa imepewa jina la Marehemu Prof David Massamba mzaliwa wa Kijiji cha Kurwaki na aliyekuwa bingwa wa mabingwa wa lugha ya kiswahili.

Kazi kubwa za ustawishaji wa lugha ya Kiswahili zilizofanywa na Marehemu Prof David Massamba kwa kushirikiana na wataalamu wenzake

Yaliyofanywa na marehemu Profesa Massamba ni kuandika vitabu vinavyotumika vyuo vikuu na sekondari ni (Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu)
na uandishi wa kamusi ya kiswahili

Michango ya awali ya ujenzi iliyotolewa ni ya
wanakijiji shilingi milioni 1,870,000,familia ya Massamba shilingi 800,000,wazaliwa 2 wa Kijiji cha Kurwaki shilingi 750,000 ambao ni Dr. Rukonge Manoko na ndugu Kawawa Jackson, diwani wa Kata shilingi 200,000, wazazi wa Kijiji jirani cha Kiriba shilingi 80,000 na walimu makada wa CCM shilingi 70,000

Michango ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo mchango binafsi amechangia mifuko 250 ya saruji huku mfuko wa jimbo ukichangia mifuko 205.

Wananchi na wadau wa elimu wameombwa kuendelea kuchangia kupitis akaunti ya Kijiji cha Kurwaki iliyopo benki ya NMB kwa namba 30302301539

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema ujenzi wa sekondari hiyo itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya kuenzi kazi nyingi na muhimu sana alizozifanya Marehemu Prof David Massamba kwenye ukuzaji na usitawishaji wa lugha ya Kiswahili kitaifa na kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!