Home Kitaifa WANAFUNZI SHULE YA MUSOMA WAFIKISHIWA ELIMU YA MAADILI

WANAFUNZI SHULE YA MUSOMA WAFIKISHIWA ELIMU YA MAADILI

Na Shomari Binda-Musoma

KAMPENI ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania ( SMAUJATA) mkoa wa Mara imeendelea na ziara ya kuzifikia shule na kutoa elimu ya maadili.

Ikiwa leo ni siku ya familia duniani na kuelekea siku ya utoaji wa tuzo kwa mashujaa wa Smaujata, elimu imetolewa kwenye shule ya msingi Musoma.

Makamu Mwenyekiti wa Smaujata mkoa wa Mara Joyce James, amesema wanafunzi wanapaswa kufikishiwa elimu ili kutambua madhara ya ukatili wa kijinsia na kujiepusha na vitendo vya ushoga na usagaji.

Amesema kukosa maadili ndio chanzo kikubwa cha wanafunzi wengi kupelekea kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.

Joyce amesema kama mkazo usipowekwa katika utoaji wa elimu vijana wengi wataaribikiwa wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Amesema Smaujata mkoa wa Mara imejipanga kuzifikia shule zote kufikisha elimu ili kuwa na jamii ambayo itaishi bila ukatili.

Leo tumefika hapa shule ya msingi Musoma kutoa elimu ili nanyi wanafunzi muweze kutoa taarifa mnapoona vitendo vya ukatili”

Msiogope kutoa taarifa pale mtakapoona mtu yoyoye anataka kuwafanyia vitendo vya ukatili kama ambavyo vimeelezwa leo”, amesema Joyce.

Mkuu wa shule ya msingi Musoma,Dominic Charles, ameishukuru Smaujata mkoa wa Mara kwa kufikisha elimu shuleni hapo ili kuiokoa jamii.

Katika utoaji elimu huo Makamu Mwenyekiti wa Smaujata mkoa wa Mara aliambatsna na viongozi wengine wa taasisi hiyo wilaya ya Musoma na mkoa wa Mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!