Home Kitaifa WANAFUNZI MSIOGOPE KUSOMA VYUO VYA NJE

WANAFUNZI MSIOGOPE KUSOMA VYUO VYA NJE

Na Magrethy Katengu

Watanzania wameshauriwa kutoogopa kuwapeleka watoto wao kusoma vyuo vikuu vya nje ya nchi kwa kuhofia gharama kubwa za mahitaji mbalimbali ikiwemo ada na fedha za kujikimu.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kampuni ya Global link,Abdulmalik Mollel alipokuwa akimwelezea waziri wa elimu sayansi na teknolojia,Prof Adolf Mkenda wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika ufunguzi wa maonesho ya 18 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yenye kauli mbiu isemayo “kukuza elimu nchini kupitia elimu ya juu,sayansi na teknolojia kwa uchumi imara na ushindani”yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 17 hadi 22,2023.

Amesema kampuni hiyo inayojihusisha uwakala wa kupeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi ina vyuo bora 14 vya gharama nafuu ikiwemo katika nchi za Uturuki,India,Canada na Malawi ambapo amesema wanatamani waone sylabus za kitanzania zikifundishwa katika vyuo hivyo.

Akiitolea mfano vyuo vikuu bora vya nchini India ambavyo hufundisha masomo ya uhandisi kwa gharama nafuu,Abulmalik amesema mwanafunzi anayepata bahati ya kujiunga na vyuo hivyo hutumia dola 510 kwa ajili ya chakula mwaka mzima huku ada ikiwa ni dola 1500 ambayo mtanzania anaweza kumgharamia mwanafunzi kwa kulipa kidogo kidogo mpaka mtoto wake atakapohitimu mafunzo yake.

Tunatamani mafunzo ya kozi za uhandisi wanafunzi waweze kwenda kusoma nje ya nchi ili wapate teknolojia mpya hivyo tunaweza kuwaomba wazazi wawalete watoto wao hapa glaballink ili tuwafanyie udahili na wasiogope kiingereza kwani ni sawa na kile walichofundishwa mashuleni hapa nchini” amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!