Home Kitaifa AAT KUTOA SEMINA YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI

AAT KUTOA SEMINA YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI

Na Magreth Mbinga

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Meloe Buzema amewataka wanafunzi kuacha kucheza barabarani wakati wanatembea wakiwa makundi ili wasipate madhara au kupoteza maisha kwa kugongwa na gari.

Amezunguamza hayo na wanafunzi wa sekondari na msingi Mnazi mmoja katika hafla iliyoandaliwa na Taasisi ya AAT yenye lengo la kuhamasisha madereva kuendesha Km 30 kwa saa sambamba na utoaji wa semina ya elimu ya usalama barabarani.

Aidha Kamishana Buzema amesema uendeshaji huo wa Km 30 kwa saa huendeshwa zaidi kwenye maeneo ya shule na makazi ya watu kwa semina hiyo wanafunzi watakuwa mabalozi kwa wanafunzi wenzao na jamii kwa ujumla ili kuepusha ajali.

“Mchango mkubwa wa ajali za barabarani ni mwendokasi ambao husababisha ulemavu na vifo hivyo elimu hii ya kuendesha Km 30 kwa saa tutaipeleka kwa madereva ili kuendesha maeneo ya huduma za jamii kama vile shuleni makazi, masoko, hospital, nyumba za ibada na maeneo mengine mengi ambayo hukusanya watu wengi “amesema Kamishna Buzema.

Pia Naibu Meya wa Ilala Ndugu Saadi Kimji amesema anaishukuru taasisi ya AAT kwa kujitolea kutoa elimu hiyo ya usalama barabarani wao kama wadau wanashirikiana vizuri na taasisi za Serikali kuhamasisha utii wa sheria bila shuruti.

“AAT bado wanaendelea kutoa michango mbalimbali kuhusu usalama kwa kutoa alama za usalama leo wamekusanya wanafunzi na kuwapatia elimu ili wakawe mabalozi kwa wenzao na jamii zao wanazotoka “amesema Kimji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!