Na Magreth Mbinga
Wagombea 306 wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea uongozi wa CCM ngazi mbalimbali katika wilaya ya Ilala ambapo zoezi hilo lilianza tarehe 2 mwezi wa 7na kutamatika tarehe 13 mwezi wa 7.
Hayo yamezungumzwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Iddi Mkowa na kusema kuwa watu 12 wamechukua fomu kugombea nafasi ya Mwenyekiti CCM Wilaya kati yao wanaume 11 na mwanamke 1.
“Watu 15 wamejitokeza kuwania nafasi ya Katibu wa Siasa na Ueneza kati yao wanaume 13 na wanawake 2,wanaowania nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri kuu wamejitokeza 153 kati yao Wanaume 109 na Wanawake 44″amesema Mkowa.
Pia Watu 91 wanawania nafasi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kati yao Wanaume 83 na Wanawake 8 na Watu 35 wamejitokeza kuwania nafasi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa ambapo kati yao Wanaume 27 na Wanawake 8.
Sanjari na hayo Mkowa amesema zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu linaendelea vizuri na kuwataka wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi Katibu Mkuu ameongeza siku ili watumie nafasi yao Kikatiba.