Home Kitaifa WANACHAMA BIASHARA UNITED WAKUBALI KUITOA TIMU KWA MDAU WA MICHEZO BILA MASHARTI

WANACHAMA BIASHARA UNITED WAKUBALI KUITOA TIMU KWA MDAU WA MICHEZO BILA MASHARTI

Na Shomari Binda-Musoma

WANACHAMA wa timu ya Biashara United ” Wanajeshi wa Mpakani” wameridhia kuitoa timu hiyo kwa mdau wa michezo Richard Sakala bila masharti.

Kwa kauli moja kwenye kikao cha wanachama kilichofanyika leo januari 18 wamelidhia kuitoa timu hiyo.

Mwenyekiti wa muda wa timu hiyo Gabriel Ipyana amewaambia wanachama wamempata mdau ambaye yupo tayari kuibdesha timu hiyo na kutaka baraka za wanachama.

Amesema mdau huyo yupo tayari kulipa kiasi cha milioni 71 ikiwa ni madeni ya mishahara ya wachezaji,benchi LA ufundi na waliotoa huduma kwenye timu.

Ipyana amesema mdau huyo amekuja wakati muafaka na kuwaomba wanachama kulidhia na kumkubalia.

” Ndugu zangu tumepitia kipindi kigumu hapa katikati katika kuiendesha timu lakini nafuraha kuwapa taarifa ya kupata mdau wa kutusaidia,

” Yupo tayari kuiendesha timu na itaendelea kubakia mkoani Mara na kuutumia uwanja wa kumbukumbu ya Karume”,amesema.

Kwa upande wao kwa kauli moja wanachama wa timu hiyo wamesema hawana kipingamizi na kumuomba mdau huyo kufika Musoma kwaajili ya kukabidhiwa rasmi.

Zawadi Ruta mmoja wa wanachama waliohudhuria kikao hicho wameshukuru uongozi kwa jitihada za kupata mdau huyo ambaye yupo tayari kuiendesha timu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!