Home Kitaifa WANA LUDEWA WASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA RAIS SAMIA,DC AANDAA FUTARI YA PAMOJA

WANA LUDEWA WASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA RAIS SAMIA,DC AANDAA FUTARI YA PAMOJA

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva,ameungana na wananchi wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe katika Dua Maalumu ya Kumuombea Kheri na Baraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika Msikiti wa Wilaya ya Ludewa.

Akizungumza baada ya dua, DC wa Ludewa Mwanziva amesema kuwa, lengo la tukio hilo la Dua Maalumu ni kwaajili ya kumuombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia ni kuendelea kuitenda kazi na Mungu kumtangulia katika kila hatua na kuyaenzi mengi mazuri anayoyafanya ndani ya Wilaya ya Ludewa,Mkoa wa Njombe na Tanzania kwa ujumla.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Ludewa amendaa Futari “Iftar’ Maalumu iliyoleta pamoja waumini wa Dini ya Kiislam Wilayani Ludewa wakiongozwa na Sheikh wa Wilaya ya Ludewa Bwn. Haruna Rahim ambaye aliungana na viongozi wa Chama na Serikali Wilayani Ludewa- akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mhe. Wise Mgina, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Ndg. Stanley Kolimba- na viongozi wa Chama na Serikali Wilayani Ludewa sambamba na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wafanyabiashara na makundi maalum.

Katika hatua nyingine katka hafla hii maalum Mkuu wa Wilaya Victoria Mwanziva amempatia zawadi ya Pikipiki kwa Sheikh wa Wilaya ya Ludewa itakayo mrahisishia utoaji wa huduma kwa waumini wa dini ya Kiislam ndani ya Wilaya ya Ludewa na shughuli zake mbalimbali za kijamii Wilayani.
Sambamba na hilo DC Mwanziva amekabidhi kwa Waumini wote wa Dini ya Kiislam Wilayani Ludewa tende kwa uwakilishi wa mashekhe misikiti ya kata mbalimbali, na waumini na washiriki wote katika tukio la Futari.

Pia, Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mheshimiwa Joseph Kamonga naye amewashika mkono kwa kutoa mchango wa Milioni Moja taslim kwa ajili ya kuendelea na maboresho ya Msikiti wa Wilaya ya Ludewa.

Akihitimisha Mhe Mwanziva amesema, Tukio hilio limekuwa la kipekee na lenye kuleta pamoja jamii na kuunganisha imani zote ila limemgusa moja kwa moja Shekhe wa Wilaya na Msikiti wa Wilaya ya Ludewa na kuwashukuru wadau wote walioshiri kufanikisha yote ikiwa ni pamoja na Benki ya CRDB, Kuambiana Investment, Mhe Mbunge Ludewa, ASAS na DED Ludewa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!