Na Shomari Binda-Musoma
TIMU 2 zilixocheza fainali msimu uliopita wa Mathayo Cup,Nyasho fc na Makoko fc,zinakutana kesho kwenye robo fainali ya mwisho ya mashindano hayo.
Mshindi wa mchezo huo ataungana na timu za Nyakato, Nyamatare na Mwigobero ambazo tayari zimetinga hatua ya nusu fainali.
Mchezo huo unaosubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka mjini Musoma utafanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Mara.
Timu zote mbili zimetoa tambo ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo na kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ya Mathayo Cup.
Kocha wa timu ya Nyasho Omary Hamis ametamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kwa kuwa amewaandaa vijana wake vizuri.
Amesema mchezo wowote unahitaji maandalizi na yeye amefanya hivyo kwenye uwanja wa mazoezi.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mzawa Blog,Diwani wa Kata ya Makoko Patrick Gumbo ambaye ndiye Meya wa manispaa ya Musoma amesema benchi la ugindi lipo na litatekeleza majukimu yao vizuri.
Amesema yeye kama kiongozi aliwapa benchi la ufundi majukumu yote ya kuiongoza timu na anaamini kwa kuwa mwaka jana walipoteza ng’ombe hatua ya fainali mwaka huu watafanikiwa.
Aidha mashabiki wanaofatilia mashindano hayo wamempongeza mbunge Mathayo kwa kufanya mashindano hayo kila mwaka na kutoa burudani kwa wa kazi wa jimbo la Musoma mjini.