Wajasiriamali wadogo wadogo wamekuwa wahanga wa matukio Panya road maana wanaamka alfajiri sana ili kuwai kuchukua mizigo kwa lengo la kuuza katika masoko mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa Leo Octoba 4,2022 na Mwenyekiti wa Machinga mkoa wa Dar es Salaam Anamota Yusuph wakati akizungumza na Waandishi wa habari. Use
“Wameadhiri na kuwaumiza na kuwaumiza baadhi ya wanachama wetu katika maeneo mbalimbali ,kama mnavyojua machinga tumetapakaa katika Jiji lote,kwahiyo wanachama wetu wamekuwa wakishambuliwa katika hayo maeneo”
Aidha Mwenyekiti amelipongeza Jeshi la polisi kwa hatua za haraka za kuweka utaratibu mbalimbali katika kukabiliana na makundi hayo. Pia ametoa wito kwa jamii na wanasiasa wanaojaribu kupotosha huu mchakato maana ni janga la kitaifa
“Vijana wetu tumewasomesha tukiwa na malengo waje kuwa msaada kwa jamii. Pia tuache siasa chafu kwamba kuna kazi nzuri ambayo serikali kupitia Jeshi la Polisi na vyombo vyake wanavyovifanya,halafu makundi mengine yanakuja kuharibu amani kwenye jamii“
Naye Makamu Mwenyekiti wa machinga Tanzania Sinde amesema kuwa vijana wachagamkie fursa za kujipatia fedha za swali na sio kuvamia wamachinga na kuwapora vitu na Kisha kuwajeruhi.