Home Kitaifa WALIOKUWA WAKIISHI NDANI YA HIFADHI YA NGORONGORO WAISHUKURU SERIKALI KUKABIDHIWA NYUMBA MPYA

WALIOKUWA WAKIISHI NDANI YA HIFADHI YA NGORONGORO WAISHUKURU SERIKALI KUKABIDHIWA NYUMBA MPYA

Kiongozi wa Kimila wa kabila la Wamasai waliokuwa wakiishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, Laigwanani Tauwo ametoa shukrani kwa serikali baada ya serikali kuanza kuwakabidhi hati ya Ardhi na nyumba mpya zilizojengwa katika eneo la Msomera.

Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi bilioni 1.2 kwaajili ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa makazi kwa wananchi waliokubali kuhama kwa hiari kutoka katika hifadhi na kupewa nyumba, Ardhi na huduma bora za jamii ikiwemo miundombinu ya Elimu, Afya, Maji, Umeme n.k

Fedha hizi zinatolewa na serikali ikiwa ni adhma ya Rais Samia kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora ya kuishi na maeneo ya kufanya shughuli zao za kilimo na ufugaji bila hatari yoyote tofauti na ilivyo sasa katika maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro ambako wananchi wamekuwa na changamoto mbalimbali.
 
Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo inahusisha nyumba zaidi ya 100 ambapo idadi kubwa imekamilika katika viwango vya ubora wa hali ya juu. Hapo jana Waziri wa Maliasili na Utalii aliongoza viongozi wengine wa kitaifa katika zoezi la kuwapokea wananchi ambao tayari wameanza kuhamia katika eneo la Msomera.

Kwa kutambua shughuli za kilimo na ufugaji, Serikali tayari imeshapima viwanja 2,500 na kutenga eneo la ekari 1,700 Kwa ajili ya kilimo na malisho kwa wakaazi wa Msomera, Wilayani Handeni. Pongezi za kiongozi wa kimila ni ishara ya kujali juhudi za serikali kwa wananchi.
 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!