Home Kitaifa WALIOKIMBIA SOKO NA KUVAMIA ENEO LA BARABARA YA TANROADS MARA WATAKIWA KUONDOSHWA

WALIOKIMBIA SOKO NA KUVAMIA ENEO LA BARABARA YA TANROADS MARA WATAKIWA KUONDOSHWA

Na Shomari Binda-Musoma

WAFANYABIASHARA wa soko la Nyamatare lililopo manispaa ya Musoma wamemuomba mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kuwaondosha wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo Happynes Kennedy kwenye kikao baina ya mkuu wa Wilaya na wajasiliamali pamoja na wasafirishaji wa bodaboda na bajaj.

Katika kikao hicho kilichofanyika leo septemba 19 kwenye ukumbi wa mikutano wa manispaa Mwenyekiti huyo amesema rwanashindwa kufanya biashara kutokana na wateja kuishia barabarani lakini pia ni hatari kwa walioko nje.

Amesema ombi lao kwa mkuu huyo wa Wilaya ni kuhakikisha wale wote walioko barabarani wanatolewa na kurudi sokoni.

” Tunakushukuru mkuu wa Wilaya kwa kuamua kukutana nasi leo na sisi kama wajasiliamali wa soko la Nyamatare tunayo kero ya walioondoka sokoni na kuhamia barabarani.

” Kuhamia kwao barabarani kunafanya wateja wanashindwa kuingia sokoni lakini pia ni hatari kwa maisha yao kutokana na ajali zinazoweza kutokea”,amesema.

Akitoa majibu ya jumla kwenye kikao hicho ambacho kiliwashirikisha pia wataalam wa manispaa akiwemo afisa biashara wa manispaa ya Musoma Charles Salywugu,mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema yapo mambo ambayo ameyapata kupitia kikao hicho.

Amesema anataka kuiona Musoma ambayo haina manyanyaso na kila mmoja anafanya biashara kwa kuzingatia utaratibu na kunufaika kiuchumi na kulipa mapato ya serikali.

Kuhusu wafanyabiashara wanaofanya biashara eneo la barabara kwa kutoka sokoni ameagiza wahusika kufatilia na kuhakikisha wafanyabiashara hao wanarudi sokoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!