Home Kitaifa WAKUU WA WILAYA BUNDA,MUSOMA NA BUTIAMA WAHIMIZA USHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

WAKUU WA WILAYA BUNDA,MUSOMA NA BUTIAMA WAHIMIZA USHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Shomari Binda-

WAKUU wa Wilaya za Bunda,Butiama na Musoma wamewahimiza wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kauli hiyo wameitoa leo kwa nyakati tofauti kwenye stendi ya zamani mjini Bunda kwenye tamasha la nyama choma.

Wamesema licha ya kushiriki tamasha hilo lililoasisiwa na mkuu wa mkoa wa Mara Evans Mtambi kutangaza nyama bora ya mkoa wa Mara lakini suala la uchaguzi lina umuhimu wake.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mwalimu Moses Kaegele amesema inapoliwa nyama bora ya mkoa wa Mara likumbukwe suala la uchaguzi.

Juma Chikoka mkuu wa Wilaya ya Musoma amesema ” bata” la nyama choma ya Bunda limekuwa bora lakini wananchi wakumbuke uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amesema kushiriki ni pamoja na kuhudhulia mikutano ya kampeni ya wagombea itapoanza novemba 20 hadi 26.

” Tule ” bata” la nyama choma lakini tukumbuke mbele yetu tunao uchaguzi wa serikali za mitaa twende tukashiriki kuwapata viongozi wa mitaa yetu”,amesema Chikoka.

Mkuu wa Wilaya mwenyeji wa Bunda Dk.Vicent Naano amewashukuru wakuu hao wa Wilaya kushiriki tamasha hilo nakuhamasisha uchaguzi.

Amesema mkuu wa mkoa wa Mara ameasisi jambo muhimu la nyama choma kwa kuitangaza nyama bora ya mkoa wa Mara na Bunda litakuwa endelevu.

Naano amesema kila mwananchi anapaswa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kuhakikisha wanapatikana viongozi bora.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!