Home Kitaifa BASHUNGWA: TUPO TAYARI KUFIA SITE KULIKO KUMUANGUSHA RAIS SAMIA

BASHUNGWA: TUPO TAYARI KUFIA SITE KULIKO KUMUANGUSHA RAIS SAMIA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema wako tayari kuifia site kuliko kumuangusha Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi na kusimamia utekeleza miradi ya maendeleo.

Mhe. Bashungwa ametoa kauli hiyo, mara baada ya kuapishwa kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa na kusisitiza kwenda kujipanga kubadilika na kuwa wizara inayowahudumia wananchi na kuwa wizara inayotatua kero na changamoto za wananchi kwa wakati.

Alisema asilimia 70 ya watumishi wa umma wako Ofisi ya Rais-TAMISEMI na kuwa kila mmoja akitekeleza wajibu wake inamaana utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi itatekelezwa kwa zaidi ya asilimia 70.

Alisema kwa mwaka 2022/23,Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeweza ukusanyaji mapato na kuvuka malengo kwa kukusanya mapato kwa asilimia 103 na kusisitiza kuwa bado kuna fursa kubwa ya kuongeza malengo haya

Mheshimwa Rais umetuelekeza tuhakikishe tunadhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato, timu hii iliyopo mbele yako mara baada ya kuapa, tunakwenda kujipanga na tunataka dhamira yako (Rais Samia) ya kuwahudumia wananchi kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI ikatimie, tuko tayari kufia site kuliko kukuangusha.”

Aidha, Bashungwa alimuahidi Rais kuwa timu hiyo wataekenda kutekeleza maagizo anayoyato ikiwamo ya ukusanyaji mapato na kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za miradi.

Nikuhakikishie Mheshimwa Rais hii ndio timu yako ya ushindi, umetuamini hatutakuangusha.”

Pia aliwakumbusha wakuu wa mikoa kujipanga kuhakikisha Sensa ya Watu na Makazi inafanyika kwa mafanikio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!