Home Kitaifa WAKULIMA WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ILI KUONGEZA TIJA KATIKA MAZAO

WAKULIMA WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ILI KUONGEZA TIJA KATIKA MAZAO

Na Neema Kandoro, Mwanza

KAMPUNI ya Afri Tea & Coffee Blenders wazalishaji wa majani ya chai na kahawa imewapongeza wakulima nchini kwa kulima mazao yanayotumiwa katika uzalishaji wa bidhaa zenye kiwango bora yanayochochea matumizi yake kwa watanzania.

Hayo yamebainishw jana Jijini Mwanza na Msimamizi wa Masoko Kanda ya Ziwa Said Matola akisema hatua hiyo itawezesha wakulima wa mazao ya chai na kahawa kulima zaidi ili kuwauzia.

Matola alisema kutokana na serikali ya awamu ya sita kuwekeza zaidi kwenye kilimo hapa nchini ambapo hatua hiyo itachochea ukuaji wa uchumi na kuwezesha watu kuwa na namna ya kupata vipato vyao kupitia kilimo.

“Tunaomba watanzania waongeze uzalishaji wa mazao yanayotumika kutengeneza bidhaa zetu ili nchi yetu ifikie mapinduzi makubwa kwa kilimo” alisema Matola.

Alisema kutokana na watanzania wengi kutumia bidhaa hizo zinazozalishwa Tanzania muda mrefu tangia enzi za uhuru wamekuwa wakifanya maboresho ya kiteknolojia ili kuendana na mabadiliko ya soko kutokana kuwepo kwa bidhaa toka nje.

Matola alisema wanatoa huduma zao katika mikoa ya Geita,Simiyu,Shinyanga, Mwanza na Kagera ambapo bidhaa za chai na kahawa aina ya green label, Simba Chai, Kilimanjaro tea, African pride na fricafe huzalisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!