Home Kitaifa WAKULIMA WATAKIWA KUKATA BIMA YA KILIMO ILI KULINDA MAZAO MAJANGA YANAPOTOKEA

WAKULIMA WATAKIWA KUKATA BIMA YA KILIMO ILI KULINDA MAZAO MAJANGA YANAPOTOKEA

Na Monica Sibanda

Mkurugenzi wa masoko na uhusiano Shirika la Bima la Taifa NIC Karimu Meshacki amewataka wakulima kukatia bima ya kilimo ili kulinda Mazao pindi yanapotokea majanga.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Maonesho Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema kuwa Kilimo kuwa na tija ni pamoja na kuwa na Bima Kilimo itayofanya wakati wa majanga kufidiwa kwa nguvu iliyotumika katika kulima mazao mbalimbali.

Meshack amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita Dkt.Samia Suluhu Hassan imewekeza katika kilimo hivyo NIC imekuja na Bima ya Kilimo ya kufanya Kilimo kisichokuwa na mawazo ya kufikiria majanga.

“Hatutaweza kuacha Kilimo kisiwe na Bima tutaonekana tupo kwa ajili kuua Kilimo hivyo NIC itakwenda bega kwa bega na Wakulima”

Amesema NIC inatoa Bima ya Kilimo Kwa asilimia 90 ya mazao yanayolimwa nchini na huduma za Bima zinapatikana katika Mikoa yote nchini.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano amesema kuwa wanazo Bima zingine ikiwemo ya Maisha ya kusaidia pale unapopata majanga hata kifo.

Amesema mwanaume ambaye ana Bima ya Maisha akifariki mjane anaacha kuanguaka badala yake atalia na kitambaa laini ambapo kile kilichowekwa kinakwenda kusaidia kwendesha maisha kwa waliobaki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!