Home Kitaifa WAKULIMA MARA WAELEZA MAONYESHO YA KILIMO MSETO YA V-i AGROFORESTRY YALIVYOWAINUA KIUCHUMI

WAKULIMA MARA WAELEZA MAONYESHO YA KILIMO MSETO YA V-i AGROFORESTRY YALIVYOWAINUA KIUCHUMI

Na Shomari Binda-Musoma

WAKULIMA mkoani Mara wameelezea namna walivyo nufaika na maonyesho na mafunzo ya shughuli za kilimo mseto yaliyotimiza miaka 40.

Maonyesho hayo yamekuwa yakifanyika chini ya ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la V-i Agroforestry Tanzania.

Wakizungumza kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kilimo mseto kwenye kituo cha mafunzo kilichopo Bweri wamesema maonyesho hayo yamekuwa msaada mkubwa kwao.

Wamesema kwa kipindi chote cha maonyesho hayo wamekuwa wakipata mafunzo ambayo kwa namna moja yamewasaidia kuwainua.

Mmoja wa wskulima hao kutoka wilaya ya Bunda aliyejitambulisha kwa jina la muinjilisti Saimon Julius amesema alivyokuwa akilima kipindi cha nyuma kabla ya mafunzo ni tofauti na sasa.

Amesema kwa sasa anapata mavuno mengi kwenye eneo dogo la kilimo na wakulima wengine wamekuwa wakinufaika kupitia shamba lake.

Wakulima wawezeshaji juma Hamis kutoka Musoma vijijini na Jamhuri Magoti kutoka Rorya wamesema kupitia mafunzo ya kilimo mseto kutoka kituo cha Bweri wamewezesha wakulima wengi kulima kilimo chenye tija.

“Ukiwatembelea wakulima ambao wamepata mafunzo na wale ambao hawajapata mafunzo utaona utofauti wake.”

“Familia za wakulima waliopata mafunzo zimepata nafasi ya kusomesha watoto na leo wanazisaidia familia zao kiuchumi baada ya kupata ajira maeneo mbalimbali” amesema Magoti.

Kaimu meneja wa shirika la V-i Agroforestry Monica Ndelicho amesema katika kipindi cha miaka 40 yapo mafanikio ambayo yameonekana kwa wakulima wa Tanzania na wamepanda miti zaidi ya milioni 156 na kuwa na mikakati na mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Amesema shirika linajivunia maonyesho hayo tangu yalipoanza na wakulima wanaelezea wenyewe namna walivyo nufaika na maonyesho.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonyesho hayo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na uvuvi Agnes Meena amepongeza maonyesho hayo yaliyowasaidia wakulima.

Amesema setukali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kumuinua mkulima na mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakiunga mkono juhudi hizo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maonyesho hayo yaliyoanza novemba 16 hadi 18 inasema “Palipo Stawi Miti Binadamu Ustawi ambapo yamewakutanisha wakulima kutoka mkoa wa Mara na nje ya mkoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!