Home Kitaifa WAKIMBIZA MWENGE WATAMANI KUJIFUNZA UTENDAJI KAZI KWA PROFESA MUHONGO

WAKIMBIZA MWENGE WATAMANI KUJIFUNZA UTENDAJI KAZI KWA PROFESA MUHONGO

Na Shomari Binda-Musoma

WAKIMBIZA mwenge kitaifa wamesema wanatamani kujifunza mazuri yanayofanywa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini katika kutekeleza majukumu yake.

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava wakati wa makabidhiano ya mwenge kwenye halmashauri ya wilaya ya Musoma kutoka manispaa ya Musoma leo julai 31 kwenye Kijiji cha Mmahare.

Amesema wanatambua kazi nzuri inayofanywa na Profesa Muhongo katika kutekeleza majukumu yake kama mwakilishi wa wananchi.

Kwenye eneo la mkesha wa mwenge kiongozi huyo amemzungumzia Profesa Muhongo kama mbunge anayefanya kazi na kuonekana ikiwemo kuziweka kwenye maandishi.

Amesema salamu zake kama alivyozitoa atazifikisha kama zilivyo bila kupunguza chochote kwa mheshimiwa Rais Dkt.Samia na kudai wamejifunza mazuri kwa mbunge huyo.

Akizungumzia miradi 7 waliyoitembelea kukagua na kuweka mawe ya msingi ni miradi mizuri ambayo inakwenda kuwasaidia wananchi.

Amesema wametembelea mradi wa zahanati kwenye Kijiji cha Mmahare ambayo ipo tayari kuwahudumia wananchi kwa asilimia 98 na imebakiza asilimia 2 na kuagiza kukamilishwa ili ipatekane huduma kwa asilimia 100.

Mnzava amesema wametembelea na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi ya maji yenye lengo la kumtua mama ndoo kichwani.

Kiongozi huyo amesema miradi hiyo ya maji inaendelea kuwahudumia wananchi na kudai maji hayana mbadala na kuwataka wasimamizi kuendelea kuitunza vizuri miradi hiyo.

Amesema mbio za mwenge mwaka huu licha ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inahamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa na utunzaji wa mazingira.

” Muda ukifika twende tukajiandikishe na baadae kuomba nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

” Niwasisitize wanawake na akina dada kujitokeza kuomba nafasi za uongozi na tusiwachague viongozi watoa Rushwa kwenye uchaguzi”,amesema.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kufikisha salamu kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo.

Amesema vijiji 68 vya jimbo la Musoma vijijini vyote vina miradi ya maji na wananchi wameendelea kupata maji ya bomba.

Aidha mbunge Muhongo amemkabidhi kiongozi huyo wa mbio za mwenge vitabu viwili vinavyoelezea utekeleza wa ilani ya uchaguzi kwa mwaka 2020/2022 na 2022/2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!