Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Khigoma Malima amewaarika wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika hafla ya kitaifa ya ushushwaji meli ya Mv Mwanza hapa kazi tu mwezi February 12, Mwaka huu katika bandari ya Mwanza kusini ili kujionea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Kampuni ya Huduma za meli nchini, MSCL Meja mstaafu John Mbungo amesema, kwamba tukio la Kesho ni alama kwa Taifa katika hatua ya kukamilisha Miradi ya Kimkakati.
Meli ya mv Mwanza Hapa kazi tu baada ya kesho kushushwa ndani ya maji Ziwa Victoria inatarajiwa kuendelea na matengenezo mbalimbali ya ukamilishwaji wake kabla ya mwezi june mwaka huu kuanza majaribio ya awali.