Home Kitaifa WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAENDELEA KUPEWA MAFUNZO NA JESHI LA POLISI

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAENDELEA KUPEWA MAFUNZO NA JESHI LA POLISI

Wakazi wa jiji la Mwanza wameendelea kuvutiwa na elimu inayotolewa na Jeshi la Polisi katika maonesho ya kibiashara ya Afrika Mashariki (EAC) yanayofanyika katika uwanja wa Furahisha.

Kwa nyakati tofauti wananchi hao wametembelea banda la Polisi na kuelimishwa kuhusu matumizi sahihi ya alama za barabarani kwa kutumia michoro inayoakisi barabara za jiji hilo, elimu juu ya Ukatili wa kijinsia, umuhimu wa kufuga Mbwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi na masuala mbalimbali ya kiusalama yanatolewa katika banda hilo.

Aidha, watu wa kada mbalimbali waliopata wasaa wa kutembelea viunga vya maonesho hayo, wameonesha kuvutiwa na huduma inayotolewa na Jeshi la Polisi kwani wameuliza maswali na kupewa majawabu kwa ufasaha kutoka kwa maafisa wa Jeshi hilo.

Polisi inawaomba wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika banda la Polisi kwaajili ya kupata elimu ya masuala ya kiusalama. Maonesho hayo yanatarajiwa kuhitimishwa kesho Agost 3, 2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!