Na Boniface Gideon, TANGA
JESHİ La Polisi Mkoa wa limewafikisha Mahakamani watu 5 wakazi wa eneo maalumu la kuwahamishia wafugaji Jamii ya Wamasai kutoka ngorongoro kwenda Msomera wilaya ya Handeni mkoani hapa,
Watu hao kutoka Jamii hiyo ya Kifugaji wanatuhumiwa kujihusisha na wizi wa Mifugo, huku likiwakamata wengine wawili raia wa Kenya waliokuwa wakijihusisha na wizi fedha kwenye magari.
Akitoa taatifa ya kwa waandishi wa habari kamanda wa jeshi la Polis Mkoa wa Tanga ACP Almachius Mchunguzi alisema kuwa mbali na watuhumiwa hao pia wamefanikiwa kuwakamata watu wawili raia wa Kenya waliokuwa wakijihusisha na wizi wa fedha wakiwafizia watu wakati wanatoka benki ambapo tayari wamefikishwa Mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi.
“Katika oparesheni mbalimbali ambazo tumeendelea nazo tumekamata watu ambao wamekuwa wanajihusisha na wizi wa mifugo ambao ni Kaigwa Matapeli (26), Mtemi Makulea (23), Daniel Zakayo (24) , Adam Yusuph (23) wote wakiwa ni Wamasai wakazi wa Msomera pamoja na Halid Said mkazi wa kijiji cha Mbangu wote wamefikishwa mahakamani ili waweze kujibu tuhuma zinazo wakabili” alisema Kamanda Mchunguzi.
“Tulifanikiwa kuwakamata watu wawili raia wa Kenya ambao wamekuwa wakifanya uhalifu wa pesa na mali za watu katika magali yao wamekuwa wakivizia watu wakitoka benki wanagungua na wanachukua fedha watuhumiwa hawa wamekuwa wakitumia gari aina ya İST kutekeleza wizi wao walihojiwa na kukiri kufanya makosa hayo na tayari wamefikishwa Mahakamani ili waweze kujibu tuhuma ambayo wanakabikiana nayo” aliongeza
Aidha kamanda huyo alisema kuwa katik kipindi cha mwezi mmoja september 2023 jumla ya watuhumiwa 6 wamehukumiwa kutumikia vifungo vyao hii ni mara baada jeshi hilo kukamilisha upelelezi wa makosa yaliyokuwa yanawakabili.
“Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga limefanikisha kesi 6 ambazo mahakama imeweza kuwatia hatiani watuhumiwa 9 ambao ni Ally Sabala amefungwa jela mwaka mmoja kwa kosa la kuaminiwa , Joshua Madenge ametiwa amefungwa mwaka mmoja , Christopher Mazengo amefungwa jela miezi 6, Muya Chambo amefungwa jela miezi 6 wote wakipatikana na pombe aina ya Moshi, Daniel Simon amefungwa jela miaka 12 kwa kosa la kupatikana Bangi Rashid Faki wote wakifungwa miaka 12.
“Wengine ni Selemani Ally ambaye amefungwa miaka mitatu kwa kosa la kupayikana na bangi , Ramadhani Salimu amefungwa miaka 30 kwa kosa la kuvunja nyumba usiku na kuiba na watuhumiwa wote wamepata kile ambacho wamestahili kwa mujibu wa sheria”
Pamoja na hayo Kamanda Mchunguzi amebainisha kuwa jeshi hilo linaendesha msako maalum wa kuwatafuta wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria ambapo amewataka kuzisalimisha kabla ya kufika octoba 31, 2023.
“Tumekuwa tukiendesha zoezi la kuwataka wananchi wasalimishe silaha haramu au wanazomiliki kinyume cha sheria zoezi hili lilianza tarehe 1 september ambalo litaisha 30 October 2023 niwatake wananchi ambao wanamiliki silaha visivyo halali sasa hivi wanaruhusiwa kuzisalimisha lakini baada ya hapo kuna oparesheni kali kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na isivyo halali” alisema.
Mwisho