Na Magreth Mbinga
Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania wametoa fimbo za kuwasaidia walemavu wa macho kutembea ikiwa ni kurudisha kwa jamii kama shukrani kwa Mungu kwa sababu hali wanayopitia hawakuitaka.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mkuu Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi wakati wa kukabidhi fimbo za kusaidia walemavu wa macho kutembea kutoka sehwmu moja hadi nyingine kwa viongozi wa Chama cha wasioona Tanzania Tawi la Wilaya ya Temeke.
“Tumekuja na fimbo za walemavu 20 ambazo kama wakala tumetoa kinaweza kikawa ni kitu kidogo sana kwa maana ya fedha lakini thamani yake kwa mlemavu wa macho ni kubwa sana sisi tunarudisha kwanza kama shukrani yetu kwa Mungu kwa wakala kutufikisha hapa tulipo” amesema Dkt Bitanyi.
Pia Dkt. Bitanyi amesema kwa kutoa msaada huo in kuwashika mkono wahitaji kwa namna moja au nyingine na hawataishia hapo watawagusa wahitaji mbalimbali kadiri itakavyowezekana.
Aidha Katibu wa chama cha wasioona Wilaya ya Temeke Protas Mtakyanda amesema wanayofuraha kubwa kupoke msaada huo walileta ombi lao mnamo mei 24 na Afisa mtendaji Mkuu alawapatia majibu kwamba wakala wapo tayali kuwasaidia takribani fimbo 20 kwaajili ya wanachama wao .
“Chama cha wasioona Wilaya ya Temeke ina julma ya wanachama 223 ambao ni wenye ulemavu wa macho na wote wanahitaji fimbo nashukuru kupata msaada huu kwasababu umekuja katika wakati muhimu sana kwani siku ya kesho tutaanza safari ya Mkoani Manyara kwaajili ya maadhimisho ya Kimataifa ya fimbo nyeupe ambayo chama kimeandaa kufanyia Wilaya ya Babati Mkoani Manyara” amesema Mtakyanda.
Sanjari na hayo Mtakyanda ameomba Watanzania kujipapasa ili waweze kuwasaidia kama walivyofanya Wakala ili kuwawezesha kufanya matembezi katika shughuli zao za kila siku .