Home Biashara WAKALA BORA (GUIDANCE INSURANCE AGENCY) YATUNUKIWA GARI JIPYA

WAKALA BORA (GUIDANCE INSURANCE AGENCY) YATUNUKIWA GARI JIPYA

Na Mercy Maimu
Sanlam General na Sanlam life Insurance Tanzania imemtunuku wakala wao Bora (Guidance Insurance Agency) kwa mwaka 2022 na gari jipya .Ambako Guidance Insurance Agency inawakilisha timu kubwa ambayo imekuwa mstari wa mbele kila wakati na tayari kutumika.

Akizungumzia na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja Maendeleo ya Biashara CHARLES MAGORI wakati akiwatunuku mawakala Bora zawadi ya gari na pikipiki amesema mawakala hao Bora wameshinda zawadi hizo kupitia programu inayoendeshwa na Sanlam General Insurance iitwayo Vuna point.

“Kwa mwaka mzima, Mawakala wameshinda zawadi nyingi zikiwemo pesa taslimu, pikipiki na zaidi kupitia programu inayoendeshwa na Sanlam General Insurance iitwayo Vuna point. MPANGO huu unatambua na kutunuku juhudi zinazofanywa na mawakala katika kuwahudumia wateja wa Sanlam“. amesema Magori

Ameongeza kuwa Sanlam inatoa huduma na bidhaa nyingi na kuwakaribisha wananchi wote wanaotaka kuwa sehemu ya mtandao wao mkubwa na kuhaidi kukua pamoja nao

Sanlam inatoa huduma na bidhaa nyingi ikijumuisha bidhaa zao Bora kama bima ya gari,bima ya nyumba na bima ya kusafiri. Bidhaa zingine ni bima ya Kilimo,uhandisi,baharini,vifurushi,moto na zaidi”. Aidha tunawaalika wote wanaotaka kuwa sehemu ya familia hii kubwa,piga simu 0807502336 na uwe wakala wetu” amesema Magori.

Nae mmoja wa wakala Bora ameishukuru Sanlam General Insurance kwa kumtunikia gari na kusema gari Hilo atalitumia katika biashara zake za uwakala.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!