Home Kitaifa WAKAAZI NYALUHAMA WAOMBA KUFUKIWA KWA SHIMO

WAKAAZI NYALUHAMA WAOMBA KUFUKIWA KWA SHIMO

WAKAZI wa Nyaluhama kata ya Buhongwa Jijini Mwanza wameomba Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwasaidia kufukia shimo linalohatarisha usalama wa watu katika eneo lao lililosababishwa na uchimbaji wa udongo kwa ujenzi wa barabara ya kwenda Shinyanga.

Wito huo wametoa leo katika eneo hilo ambapo kulichimbwa udongo kwa ajili ya ujenzi wa barabara na kusababisha shimo kubwa ambalo limekuwa likisababisha watu kuzama na kupoteza maisha.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Yusuf Msalangi alisema kuwa wamekuwa wakifanya jitihada wenyewe za kufukia hata hivyo imewawia vigumu kutokana na ukubwa wake na hivyo kuomba TARURA ambao wameanza ujenzi wa barabara ya lami kutoka Buhongwa kwenda Igoma kupitia Kampuni ya Zhongmei Group kusombea udongo wanaoparua katika eneo hilo.

“Tumeamua eneo hilo tujenge ofisi yetu ya Mtaa kwa ajili ya kuongeza ulinzi na usalama kwa watu wetu na tumetoa ombi letu la kusaidiwa kwa uongozi wa wilaya ili udongo unaotolewa katika ujenzi wa barabara iendayo Igoma umwagwe katika shimo hilo” alisema Msalangi.

Meya wa Jiji la Mwanza Constantine Sima amesema wanasubiri kukamilika kwa matengenezo ya katapila hivyo wataanza mara moja kutupia taka kwenye shimo hilo ili kuondoa changamoto hiyo kwenye eneo hilo.

“Tukimwaga taka tutawahi kuziba shimo hilo kwa muda katapila lilikuwa na hitilafu kwa sasa limetengenezwa hivyo tutaanza kumwaga kifusi cha taka katika eneo hilo” amesema Sima.

Mkaazi wa eneo hilo Salum Manase alisema kutokana na shimo hilo kujaa maji kipindi cha mvua imekuwa ikisababisha adha na kuhatarisha maisha ya watu katika eneo hilo hivyo kuomba serikali isaidie kutatua changamoto hivyo.

Naye Flora Luge alisema maji yanayotuwama kwenye shimo hilo yamekuwa yakitumiwa na watu kwa matumizi ya nyumbani huku yakiwa si salama na kuomba serikali iwasaidie kufukia shimo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!