Home Kitaifa WAJUMBE RCC,TANGA WATAKA KASI UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

WAJUMBE RCC,TANGA WATAKA KASI UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

Na: Boniface Gideon – Tanga

Wajumbe wa Kamati ya ushauri Mkoa wa Tanga, mwishoni mwa wiki wameketi kujadili hoja mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara zilizo chini ya Wakala wa Barabara Nchini ( TANROADS ) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini ( TARULA ) huku wakitaka kasi ya ujenzi kuongezwa kwabaadhi ya maeneo ikiwamo barabara ya Tanga- Pangani, Handeni – Kilindi pamoja na daraja la Pangani.

Aidha wajumbe hao wamepitisha ombi la bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 ya shilingi bilioni 415 kwa ajili ya matumizi ya mwaka mkoa wa Tanga.

Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini Mhe. John Sallu ambaye pia alikuwa ni mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ilizipongeza mamlaka zinazosimamia ujenzi wa miundombinu ya barabara TARULA na TANROADS kwakuwezesha maeneo mengi ya mkoa wa Tanga kupitika muda wote,

” Tanroads na Tarula mmejitahidi sana kwa kutuboreshea miundombinu ya Barabara ambapo nyingi zinapitika, lakini tunaomba muongeze kasi kwenye baadhi ya maeneo, tunataka barabara ya Handeni-Kilindi mpaka mikoa ya jirani ikamilike kwa haraka ,lakini pia Barabara ya Tanga – Pangani pamoja na ujenzi wa daraja kubwa pale Pangani, kasi bado hairidhishi” Alisisitiza Sallu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Pangani. Mhe. Akida Bahorera alizitaka Tanroads na Tarula kuhakikisha wanamalizia barabara zote kabla ya mwaka 2025 ili kupunguza maswali ya wananchi,

“Tunaomba mmalizie barabara zote hasa zile ambazo mlizianza, pale Pangani bado hatufurahishwi kiukweli, tunazo barabara za vijijini nazo tuziangalie maana tunaenda kwenye mvua za masika” Alisema Akida

Nae Francis Komba Mwenyekiti wa Halmshauri ya Korogwe Mji alisema licha ya barabara nyingi kupitika lakini Kuna maeneo yanatakiwa kuwekwa madaraja makubwa kabla ya mvua za masika hazijaanza kunyesha,

“Mvua za Masika zitaanza wakati wowote kuanzia sasa na tunatakiwa tuchukue tahadhari ili yasije yakatokea ya wenzetu, kwahiyo hakikisheni mnaweka madaraja Makubwa ili maji yapite bila kikwazo kuepusha mafuriko” Alisema Komba

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!