Home Kitaifa WAJUMBE KATA YA KISEKE WAMUONDOA DIWANI KIBABE

WAJUMBE KATA YA KISEKE WAMUONDOA DIWANI KIBABE

Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kiseke wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza umemkataa diwani wa kata hiyo Mwevi Ramadhani kwa kupiga kura za siri, ambapo kura 18 zimemtaka kuendelea huku kura 68 zikipinga kuendelea kuwa diwani wa kata hiyo.

Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kiseke Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wamuondoa Diwani wa kata kuendelea kuwa katika nafasi yake kwa kupiga kura 68 za siri kwa kushindwa kutekeleza ilani ya chama hicho.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Kiseke wamesema wamemuondoa diwani kutokana na kutotekeleza ilani ya chama hicho kutokana na kushindwa kusimamia miradi mbalimbali katika kata hiyo ikiwemo baadhi ya miradi kuitekeleza mwenyewe bila kufuata taratibu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!