Home Kitaifa WAISLAM WASHAURIWA KUTUMIA MWEZI RAMADHANI KUFANYA TOBA

WAISLAM WASHAURIWA KUTUMIA MWEZI RAMADHANI KUFANYA TOBA

Na Magrethy Katengu

Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh Dkt Abubakar Zuber Bin Ali amewaomba Waislamu wote katika kipindi chote cha Mwezi wa Mfungo wa Ramadhani kuacha kufanya matendo yasiyompendeza Mwenyezi Mungu badala yake kufanya toba na kutoa sadaka kwa makundi ikiwemo kwa makundi ya Yatima,walemavu,wazee ili wajipate thawabu nzuri kwa Mungu.

Ushauri huo ameutoa leo Jijini Dar es salaam wakati wa zoezi la ufunguzi wa ugawaji wa sadaka ya futari katika Msukitu wa Kinondoni ambapo amesema kwa mujibu ya mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W) ni suna kuwapa sadaka watu ambao hawana uwezo kwa lengo la kuwafariji na kuungana katika swala zima la kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na amesisitiza Waislamu mwezi huu wautumie vizuri kufanya toba kwa Mungu wao na aikubali funga yao na kupata thawabu bora

“Leo Waislamu wote tunasubiria Muandamo wa Mwezi hivyo wote tusione kuwa uzito Wala kimoja ibakie furaha kwa kuwa kufunga ni mojawapo ya nguzo ya Imani ya Uislamu hivyo lazima mwezi huu kutimiza masharti yake na suna yake “amesema Mufti

Hata hivyo amesisitiza mwezi wa Ramadhani utumike kufundisha maadili mema ikiwemo Subira,Ustahimilivu,huruma,Upendo,ukarimu,utoaji sadaka kwa yatima,wajane,walemavu na hata wale wasio na uwezo wa kununua vyakula kwa ajili ya futari au daku kwani kufanya hivyo ni kujipa kwa kila mmoja wao uanze kufunga suala la ugawaji wa futari na daku.

Naye Mkurungenzi wa kitengo Cha Dawaa na Tablghii Shekh Arif Suriya amesema sadaka hizo wanazozitoa hazitaishia hapo ni muendelezo kwa kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kuungana mkono kusaidia watu sadaka ya futari na daku.

“Tumezunguka katika baadhi ya miskiti na kugundua kuwa waislamu waanatofautiana muda wa kuswali hivyo tumeamua kuandaa kalenda inayooneshwa wakati sahihi wa swala kwa mikoa yote ili kuepusha waumini kula daku kabla au baada ya wakati “,amesema Shekh Arif .

Aidha Shukrani zimetolewa Kwa wale wote waliokuja kuchukua sadaka kwani bila hivyo zoezi hilo lisingefanikiwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!