Home Kitaifa WAHITIMU JKT WATAKIWA KUWA WAZALENDO NA MOYO WA KULITUMIKIA TAIFA.

WAHITIMU JKT WATAKIWA KUWA WAZALENDO NA MOYO WA KULITUMIKIA TAIFA.

NA BONIFACE GIDEON, TANGA

WAHITIMU wa Jeshi la Kujenga Taifa Nchini JKT kikosi 838 KJ Maramba mkoani Tanga wametakiwa kuwa Mabalozi, Wazalendo na Moyo wa kuitumikia Nchi yao pamoja na kulinda na Kudumisha Amani ya Nchini na Kusaidia Serikali kutatua migogoro ya Wananchi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Kanali Maulid Surumbu Wakati akifunga Mafunzo ya Jeshi Hilo kwa Mujibu wa Sheria oparesheni Venance Mabeyo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Jeshi Hilo lililopo Tarafa ya Maramba na kuhudhuriwa na Mamia ya Wananchi, Wazazi, Walezi na Viongozi mbalimbali wa Kijeshi na Serikali.

Kanali Maulid Alisema Mafunzo waliyoyapa Wanatakiwa kuyatumia kwakuwa mfano kwenye Jamii ikiwamo kwenye uzarishaji ,

“Tunarajia Mafunzo haya yatakuwa na tija Kwenye kwenu na Taifa kwaujumla, Nendeni mkaisaidie Jamii kutatua migogoro na msiwe chanzo Cha Migogoro kwenye Jamii pia mkawe na Uzalendo na moyo wakuitumikia Nchi yenu” Alisisitiza Maulid Surumbu

Alisema Taifa linategemea nguvu kazi ya Vijana wakiwamo wanaohitimu JKT ,

” Taifa letu linategemea nguvu kazi ya Vijana mkiwemo ninyi mnaohitimu JKT hivyo, Serikali inamatarajio makubwa kwenu na ndio Mana imetumia gharama kubwa ya kuwaandaa na kufika hapa mlipofika” Alisisitiza Kanali Maulid Surumbu

Kwaupande wake mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Nchini JKT Kanali Aisha Matanza aliwataka Wazazi/ Walezi kuwaruhusu Watoto wanapopata nafasi ya kujiunga na Jeshi Hilo kwaajili ya kupata Mafunzo

“Kwa Wazazi Niwaombe Muwaruhusu Watoto wenu pale wanapopata nafasi ya kujiunga na Jeshi letu , Mafunzo haya ni Mazuri wenyewe mmejionea walivyokuja sivyo wanavyotoka, wamejifunza vitu vingi ambavyo vitawasaidia wao na Taifa letu na Niwaombe pale mtakapo hitajika kutumika na Taifa msisite kujitokeza” Alisisitiza

Aliwataka Wahitimu hao kudumusha Nidhamu na kulinda Afya zao,

” Ujana ni kuwa na Afya Bora, Nendeni mkalinde Afya zenu ikiwamo kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuharibu Afya zenu ikiwamo uvutaji wa Sigara Matumizi ya Dawa za Kulevya pia mkadumishe Nidhamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!