Neema Kandoro Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limewakamata waganga wa kienyeji 33 wanaojihusisha na ramli chonganishi na kufanya shughuli za uganga wa kienyeji bila kufuata taratibu za kisheria na kukutwa na vielelezo mbalimbali pia linawashikilia wanaume 5 kwa kosa la kuruhusu miili yao kuingiliwa kinyume na maumbile.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Wilbrod Mutafungwa alisema tarehe 17 Mwezi huu kwa nyakati tofauti tofauti katika kijiji cha Igunguya Wilaya ya Kwimba waliwakamata Lunyilija Ndila (51) Mkazi wa Kijiji cha Igunguya, Mashaka John (36) mkazi wa kijiji cha Bungulwa na Ngeneja Kisinza (45) mkazi wa Kitongoji cha Kilyaboy
Kamada Mutafungwa aliseama tarehe 24 Mwezi huu katika Kitongoji cha Keseni Kijiji cha Kigongo Wilaya ya Misungwi walifanikiwa kuwakamata Samson Fransis(40) Mkulima na Mkazi wa Kitongoji cha Kasenyi, John James(59) Mkazi wa Igunga, Richard Ngusa (52) mkulima na mkazi wa Igunga. Bujikano Zabron (60) Mkulima na Mkazi wa Mwamazengo, Ngwalu Madilisha (60) Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Misasi, Makoye Stephano (40) Mkazi wa Kijiji cha Nyamantale pamoja na Kahabi Sylivesta (51) Mganga wa Kienyeji na Mkazi wa Misungwi
Hemed Aloyce (24) Mganga wa kienyeji na Mkaziwa Kisesa, Hellena Mwanzalina (61) Mganga wa Kienyeji na Mkazi wa Nyanguge, Maduhu Kinanai (23) Mganga wa kienyeji na Mkazi wa Kisesa pamoja na Masai Jacob (36) Mganga wa kienyeji na Mkazi wa Nyanguge.
Kamanda aliongeza kuwa Tarehe 24 Mwezi huu katika Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Ngoma ‘A’ Kata ya Igalula tarafa ya Nyanchenche Wilaya ya Sengerema waliwakamata Kazmil Kaboja (75) Mkulima Mkazi wa Kitongoji cha Mlimani, Faida Fundikila (55) Mkazi wa Mwabaluhi, Maritha Ibalaja ( 55) Mkulima Mkazi wa Mwabaluhi, Kulyalya Idubulilo (57) Mkazi wa Isunghanholo.
Katika hatua nyingine Kamanda Mutafungwa alisema tarehe 24 Mwezi maeneo ya Uniquie Saloon Kta ya Buzuruga na Nyamuge Wilaya ya Ilemela kwa nyakati tofauti tofauti waliwakamata vijana wa kiume Ramkhity Balkhabaty (26) Mkulima na Mkazi wa Buzuruga.
Daniel Omary (24) Mkulima na Mkazi wa Buzuruga , Ernest Malongo (20) Mkulima na Mkazi wa Mecco, Jefta Joseph (27) Mkulima na Mkazi wa Kisesa pamoja na Edward Abel (30) Mfanyabiashara na Mkazi wa Nyamuge kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile
Ofisa Mhifadhi Wanyamapori Daraja la Kwanza Kanda ya Ziwa Omar Mpita amewataka waganga wa tiba asili kujisajiri katika Ofisi za Utamaduni ili wapatiwe vibari ili kuwatambua kisheria
Naye Wakala wa Huduma za Misitu ( TFS) Kanda ya Ziwa Emanuel Mgimwa amewataka waganga wa jadi nchi kuacha tabia ya kuvamia misitu na kuchimba mizizi pamoja na kun’goa magome ya miti kwa kigezo chakutafuta dawa.
“Niwashauri waganga ni vyema wakaandaa vitalu vya miti ambayo hutumia kwenye tiba zao ili kuwarahisishia upatikanaji wa dawa zao na pia itasaidia katika kulinda uhifadhi wa misitu nchini.” Alisema