Home Kitaifa Wafugaji samaki kwa vizimba Kanda ya ziwa kunufaika na mikopo ya bilioni...

Wafugaji samaki kwa vizimba Kanda ya ziwa kunufaika na mikopo ya bilioni 60

Na Neema Kandoro Mwanza

MAKUNDI ya ufugaji samaki kwa vizimba katika kanda ya ziwa yataanza kunufaika na mkopo usio na riba wa Sh bilioni 60 uliotolewa na serikali kuwezesha kuwepo kwa ongezeko la samaki na kutoa ajira kwa wananchi.

Katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wanakikundi wilayani Ilemela jana Ofisa Uvuvi Mwandamizi Wizara ya Mifugo na Uvuvi sekta ya Uvuvi Fadhi Riziki aliwataka wanavikundi hawa wakasimamie kwa weledi mkubwa jukumu la ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kwani kwa sasa kuna upungufu wa samaki.

Riziki alisema kuwa tayari serikali imeshatoa kiasi cha pesa hicho kwa benki ya Maendeleo ya Wakulima Tanzania (TABD) kwa ajili ya vikundi hivyo katika mikoa ya Mwanza , Simiyu na Geita.

Alibainisha kuwa kiasi cha Sh bilioni 20 zimetengwa kwa ajili ya vizimba, vifaranga huku bilioni 39 kununulia boti na mahitaji mengine kwa miradi hiyo katika mikoa hiyo.

Serikali itaendelea kuwezesha makundi yote ya kijamii kwa kuwapatia mikopo ya kuanzisha ufugaji samaki kwa vizimba ikiwa ni pamoja na wazee” alisema Riziki.

Alisema kuwa mikopo hiyo ni endelevu na wanatarajia kuanza kukaribisha maombi ya wanakikundi wengine wa ufugaji wa samaki kwa vizimba hapo mwezi agasti mwaka huu na kwa sasa watalaamu wa benki ya TABD watanza kutembelea vikundi hivyo vilivyo maliza mafunzo kutoa mikopo hiyo.

Riziki alisema kuwa mkoa wa Mwanza una vikundi 36 na kwa sasa wameshamaliza kuwapatia mafunzo ya ufugaji samaki kwa njia ya vizimba ndani ya ziwa Victoria.

Mmoja wa wanakikundi cha Samaki ni Lishe kutoka mtaa wa Kigala Kata ya Buswelu Sangija Sylivester aliishukuru serikali kwa kuanzisha utoaji wa mitaji kwa ajili ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba akisema hatua imekuja muda mwafaka kutokana na kupungua kwa samaki.

Alisema fursa hiyo amewafanya hata wao vijana kuingia katika mchakato wa kunufaika na uchumi wa bluu katika eneo lao hivyo kuona mwanzo wa kukua akiwa milionea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!