NA BONIFACE GIDEON, TANGA
WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Leo wametoa msaada wa Vifaa mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia akina Mama Wajazawazito,Waliojifungua na kutoa zawadi kwa Watoto wachanga waliozaliwa hospitalini hapo.
Msaada huo wenye thamani ya Mil.2 umewafikia zaidi ya wahitaji 100 na unatokana na michango ya Wafanyakazi hao ikiwa ni Sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa Wateja yanayoendelea maeneo mbalimbali Nchini.
Akizungumza hospitalini Wakati wa Makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye wodi za akinamama , Meneja wa Tawi la NMB Madaraka Elizabeth Chawinga Alisema Wafanyakazi wa Benki hiyo wameamua kujichangisha na kutoa msaada huo kwa lengo la kurudisha fadhira kwa Jamii lakini pia kuwahamasisha Wazazi kuwafungulia Watoto wao Akaunti maalumu za kuweka akiba kwaajili ya baadaye ,
” Tumeleta msaada huu, hii ni michango yetu Wafanyakazi kwa ajili ya kurudisha fadhira kwa Jamii.