Home Kitaifa WAFANYABIASHARA YA SOKO KUU BABATI WATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG’

WAFANYABIASHARA YA SOKO KUU BABATI WATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG’

NA. MWANDISHI WETU

Uongozi wa chama cha wafanyabiashara ndogondogo kutoka Soko Kuu la Babati wamekabidhi misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe yaliyotokea mlima Hanang’ Mkoani Manyara

Disemba 3, 2023.
Wafanyabiashara hao wamekabidhi bidhaa mbalimbali ikiwemo nyanya, matunda, mboga za majani, nguo, sabuni na pesa kiasi cha Shilingi laki moja.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao, kiongozi wa umoja huo maarufu kwa jina la mama Singida alitoa salamu za pole pamoja na kukabidhi misaada iliyopokele na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi katika Ofisi Halmashauri ya Hanang’ mkoani Manyara.

Akitoa neno la shukran Katibu Mkuu huyo amewapongeza wafanyabiasha hao kwa kuona umuhimu wa kujitolea na kutoa vitu vitakavyosaidia mahitaji ya waathirika hao huku akiendelea kuwaomba wadau kujitokeza zaidi
“Kipekee ninawashukuru sana, hili ni jambo jema kuwakumbuka wenzetu walipata maafa haya, na misaada yenu itawafaa sana hususan masuala ya chakula na viungo vya jikoni, mmefanya vyema sana,” alisema Dkt. Yonazi


=MWISHO=

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!