Home Burudani WADHAMINI WAOMBWA KUDHAMINI USIKU WA WAFIA DANSI

WADHAMINI WAOMBWA KUDHAMINI USIKU WA WAFIA DANSI

Mratibu wa tamasha la Usiku wa Wafia Dansi bwana Bernard James amewaomba wadhamini kujitokeza kwa wingi kudhamini tamasha hilo ili lifane zaidi

Tamasha hilo lenye lengo kubwa la kukuza muziki wa dansi, kutoa ajira, kukuza sanaa, kuleta ubunifu na ushindani kwenye dansi, kuutangaza muziki wa dansi na kutoa burudani litafanyika jijini Dodoma mwezi wa 8

Bernard amesema wadhamini wakidhamini tamasha hilo watatangazwa kwenye redio, TV, mitandao ya kijamii, kwenye mabango, kushiriki vipindi mubashara, kujitangaza siku ya tamasha pamoja na kuuza bidhaa, jina, kupata wateja wapya na kujenga taswira nzur zaidi

“Matangazo mengi unayaona kwenye mitandao kibao ya kijamii hasa WhatsApp, Instagram, Facebook, YouTube huku mengine yakipigwa redioni, pia siku ya tamasha litarushwa live kwenye kituo kikubwa cha Star TV, sasa hapo huoni wadhamini watapata faida kubwa?”

Bernard amewaomba wafanyabiashara wakubwa, wadogo, wa kati pia wajasiriamali kuitumia vyema fursa ya tamasha hilo kufanyika jijini Dodoma kujinadi

“Watanufaika zaidi maana sikukuu ya wakulima 8,8 kitaifa itafanyika mkoani Dodoma, sasa wanaweza tumia fura hiyo kutangaza na kuuza bidhaa, huduma, brand na kueleza mafanikio na mipango yao kupitia tamasha hilo”

Bernard amesema mpaka sasa wadhamini waliodhamini ni Star TV, Redio Free Afrika, Kiss FM, Cheza Kidansi, BJ Fashion, C FM, Royal Village Hotel Dodoma.

Tamasha la Usiku wa Wafia Dansi liliasisiwa mwaka 2018 jijini Dar es Salaam kisha likafanyika mfululizo katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam na Dodoma.

Litafanyika tarehe 2 Agosti siku ya Ijumaa jijini Dodoma kwa mara ya pili katika ukumbi wa Royal Village viingilio vikiwa shilingi 10,000, 30,000 na 500,000 ambapo bendi 5 za jijini Dodoma za Sky Melodies, Perfect Music, TNC band, Gold Musica na JKT Makutupora Music Band zitapambana jukwaani kumpata mfalme wa dansi Dodoma.

Namba ya udhamini ni 0763749286

19/7/2024

CK

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!